Kumi Muhimu

Hot Reads

USIANZISHE BIASHARA KABLA HUJAFANYA HAYA KUMI.

1.Fanya utafiti wa kutosha juu ya biashara unayotaka kuazisha sio tu kwa kuwa kuna mtu unayemjua amefanikiwa kutokana na biashara hiyo. Pia hakikisha unajua ni nini utakifanya endapo biashara hiyo itaanguka ghafla.

2.Uwe tayari kufanya maamuzi magumu! Daima kuwa mtu wa kuthubutu na usiogope hasara kwani mafanikio huanza kwa taratibu na hasara ni njia moja wapo ya kujifunza na kuendelea mbele katika biashara.

3.Mafanikio huanza kwa kiasi kidogo cha fedha,  usiache kuthubutu kwa kuwa tu, hauna mamilioni ya pesa ya kuanzia kama mtaji. Siku zote hakikisha una fedha za dharula na kamwe usitumie fedha ya mtaji kwa matumizi mengine.

KAMA MPENZI WAKO YUKO FACEBOOK, ACHANA NA HAYA KUMI

 1.Kuendelea kutunza “status”  isemayo kwamba hauna mpenzi  yaani “single”. Au “Its  complicated” wakati tayari uko  kwenye mahusiano.
 2.Kuendelea kuwa na picha za mwenza wako ulieachana nae (ex) facebook kutamuumiza mpenzi wako na kusababisha migogoro wakati mwingine.

UNAMJUA VIZURI IDI AMINI WA UGANDA? SOMA MAMBO HAYA 10 UBAKI MDOMO WAZI!

1.Aliwahi kuwa bingwa wa ndondi wa uzito wa juu  nchini Uganda mwaka 1960-1961

2.alijichagua kuwa Raisi wa Uganda kwa mapinduzi ya kijeshi, na waganda wengi walimchukulia kuwa ni shujaa kwa kumuondoa raisi walieona “anasuasua” Milton Obote mwaka 1971.

3.Aliua watu zaidi ya laki tatu (300,000) kwa kipindi cha miaka 8 aliyokuwepo madarakani kabla ya Kung’olewa na Majeshi ya kitanzania mwaka 1979 baada ya kutaka kuteka sehemu ya Tanzania.

ACHA KUJIANGAMIZA! KAMA UNAFANYA HAYA UNAJIUA KIMAISHA.

1. Kujiweka wa mwisho na Kujinyima muda wa kufurahi /kustarehe
Maisha yako yamejengwa kwa  vipande vidogo vidogo ambavyo kila kimoja kina nafasi yake, na kikikosekana, basi vingine havitakaa kwenye nafasi zake na kuharibu maisha yote.

Wengi tumekuwa tunawapa nafasi wengine kwanza na kuamua kujiweka sisi wa mwisho. Matokeo yake, unajinyima muda wa kupumzika, kula, kustarehe nk! Matokeo yake huwi na furaha na maisha yako!

UNA TATIZO LA KUCHELEWA KUAMKA? TUMIA NJIA HIZI KUMI KUWAHI KUAMKA ASUBUHI

1.Kuna chakula/tunda unalolipenda zaidi? Jiwekee zawadi, kwamba ukiamka asubuhi  tu cha kwanza ni kula chakula hicho/ tunda/ chokleti nk. Hii itakufanya Utoke kitandani pale tu atakaposhtuka!

2.Iwekee Kipaumbele kazi unayopenda kufanya  zaidi iwe ya kwanza kutendeka asubuhi. Utajkuta unatamani kuamka mapema zaidi kuwahi kazi hiyo na siku yako itaenda vizuri

3.Andaa mapema nguo ya kuvaa siku inayofuatia, ili kuwahi jumatatu, andaa nguo ya kuvaa jumapili usiku. Utafiti unaonyesha kuwa asilimia 40 (40%) ya watu huchelewa kutoka kitandani kwa kuwa walitumia muda mwingi kupanga watavaa nguo gani.

WATU KUMI MASHUHURI WALIOUAWA KWA KUPIGWA RISASI (Wamo John Kennedy, Martin Luther King, 2pac na wengine)

 1.JOHN F KENNEDY (JFK)

Alikuwa raisi wa 35 wa marekani aliuwa November 22 mwaka 1963 akiwa raisi wa nne kuuawa kwa  kupigwa risasi katika historia ya marekani.  Akiwa na mkewe, kwenye gari la wazi akitoka kwenye hotuba Alipigwa risasi tatu .Mpaka leo hakuna jibu la moja kwa moja juu ya nani aliyehusika kumuua JFK japokuwa Lee Harvey Oswald ndiye aliehusishwa na mauaji hayo.Lee Harvey Oswald nae aliuawa na raia mmoja (Jack Ruby)  siku mbili tu baadae alipokuwa akipelekwa rumande. Cha ajabu ni kwamba, John kennedy, Lee Harvey Oswald, na raia aliyemuua Oswald, wote walifia katika hospitali ya Parkland Memorial Hospital kwa nyakati tofauti. Mdogo wa JFK aliyeitwa Robert F. Kennedy nae aliuawa mwaka 1968 (alikuwa anawania uraisi wa marekani)


Copyright © 2014 Kumi Muhimu