KAMA MPENZI WAKO YUKO FACEBOOK, ACHANA NA HAYA KUMI
1.Kuendelea
kutunza “status” isemayo kwamba hauna mpenzi yaani “single”. Au “Its complicated” wakati tayari uko kwenye mahusiano. 2.Kuendelea
kuwa na picha za mwenza wako ulieachana nae (ex) facebook kutamuumiza mpenzi
wako na kusababisha migogoro wakati mwingine. 3.Kuwaomba
urafiki, marafiki wa mpenzi wako kabla ya kuonana nao. 4.Kuwa
na marafiki wengi wa jinsia tofauti na kutumia muda mwingi kuchat nao
kutamfanya mwenza wako kutokuwa na imani na wewe.
5.Kum
“Tag” mtu wa jinsia tofauti picha ambayo umepiga peke yako huashiria kwamba
unataka akuone! Hii sio nzuri kwa mahusiano. Tagging humaanisha kwamba
unamtambulisha mtu uliyepiga nae picha. 6.Usipende
Kuandika ujumbe wowote kwenye ukurasa wa
mwenza wako wa zamani 7.Kuingia
kwenye profile ya mtu wa jinsia tofauti na kuanza ku ‘like’ na ku ‘comment’
picha, hii haina picha nzuri kwa mwenza wako. Kumbuka facebook hutoa taarifa ya
kila unachokifanya kwa rafiki zako. 8.Wivu
uliokithiri, hii hasa hutokea pale unapomuona mwenza wako yuko “online” alafu
hajibu message zako wala kucomment kwenye picha au status uliyotuma 9.Kutomtakia
“happy birthday” siku yake ya kuzaliwa kwenye ukurasa wake. Anaweza asikuambie,
ila atajisikia vibaya sana kupewa heri ya kuzaliwa na kila mtu isipokuwa mpenzi
wake. 10.Kutaka password ya akaunti yake ya
facebook ili kusoma ujumbe aliotumiwa. Utaumia moyo, acha!
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako