USIANZISHE BIASHARA KABLA HUJAFANYA HAYA KUMI.

USIANZISHE BIASHARA KABLA HUJAFANYA HAYA KUMI.

1.Fanya utafiti wa kutosha juu ya biashara unayotaka kuazisha sio tu kwa kuwa kuna mtu unayemjua amefanikiwa kutokana na biashara hiyo. Pia hakikisha unajua ni nini utakifanya endapo biashara hiyo itaanguka ghafla.

2.Uwe tayari kufanya maamuzi magumu! Daima kuwa mtu wa kuthubutu na usiogope hasara kwani mafanikio huanza kwa taratibu na hasara ni njia moja wapo ya kujifunza na kuendelea mbele katika biashara.

3.Mafanikio huanza kwa kiasi kidogo cha fedha,  usiache kuthubutu kwa kuwa tu, hauna mamilioni ya pesa ya kuanzia kama mtaji. Siku zote hakikisha una fedha za dharula na kamwe usitumie fedha ya mtaji kwa matumizi mengine.

4.Jitahidi kadri ya uwezo wako kupunguza matumizi yasiyo ya lazima ambayo yatapelea kuharibu mtaji wako ulioanza nao.

5.Unapokuwa unafanya mpango mkakati wa fedha jitahidi matumizi yako uyawekee makadirio ya juu na kipato chako ukiwekee makadirio ya chini.
                                                                                         
6.Kama unataka kufanya biashara na huduma ambayo kuna wengine wanafanya, hakikisha biashara yako iwe na ubora wa hali ya juu ukilinganisha na watu wengine, na ujue wanakosea wapi na utafanya nini cha tofauti la sivyo utakuwa nyuma yao milele kwani kinachowavuta watu kuja kununa kwako ni utofauti kati yako na wapinzani wako na sio tu kwa kuwa bidhaa unayo.

7.Fanya utafiti sokoni kujua watu wanazichulia vipi bidhaa au huduma unayotaka kutoa ili kuweza kujua wapi unakosea na kujirekebisha mapema iwezekanavyo ili kuendelea kutengeneza mahusiano mazuri na watu.

8.Hakikisha jina la biashara yako linamvuto na kukubalika katika jamii husika. Pia Jihusishe na watu mbalimbali walioendelea katika ujasiliamali ili uweze kupata mawazo mbalimbali na mbinu mpya za kuweza kufanikiwa katika ujasiliamali.

9.Andika! Mali bila daftari huisha bila habari. Daima tunza kumbukumbu zako katika maandishi


10.Tafuta kitu kitakachokuwa na ushawishi wa hali ya juu kwa wakati huo katika eneo husika, ukitumie kama njia ya kujitangaza. ukifanikiwa katika hilo basi utajijengea channel kubwa na watu wengi watakujua na hiyo itakurahisishia safari ya kufahamika kwa biashara yako.

1 comment:

Toa maoni yako

Copyright © 2014 Kumi Muhimu