ACHA KUJIANGAMIZA! KAMA UNAFANYA HAYA UNAJIUA KIMAISHA.
1. Kujiweka
wa mwisho na Kujinyima muda wa kufurahi /kustarehe
Maisha yako yamejengwa kwa vipande vidogo vidogo ambavyo kila kimoja kina
nafasi yake, na kikikosekana, basi vingine havitakaa kwenye nafasi zake na
kuharibu maisha yote.
Wengi tumekuwa tunawapa nafasi wengine kwanza
na kuamua kujiweka sisi wa mwisho. Matokeo yake, unajinyima muda wa kupumzika,
kula, kustarehe nk! Matokeo yake huwi na furaha na maisha yako!
2.Kukubali kuendeshwa na matukio mabaya
yaliyopita
Kuhisi kwa kuwa kuna
kitu Fulani kibaya kilikutokea kwenye maisha yako basi
maishahayatawezekana tena. Pengine ulifiwa,
kufukuzwa kazi, shule, kuibiwa au
kufilisika.
3.Kukubali
kuzungukwa na watu wasiokufaa
Ni rahisi, Siku zote watu waliokubali kushindwa,
huwa na sababu za kukupa kwa nini wameshindwa kimaisha, na ukikaa karibu nao
watakupa sababu hizi na kukufanya uamini kwamba huu ndio ukweli, na hutakuwa
tayari kupiga hatua zaidi.
4.Kukimbia
matatizo na kuogopa kushindwa
Je wajua? Ukikimbia matatizo yako, siku
zote yatakimbia pamoja nawe. Usikimbie tatizo, likabili na kuamka haraka kila
tunapoanguka. Na epuka Kuhisi kuna mtu
mwingine anahusika na furaha yako.
5.
Kuharibu Maisha ya Mwingine ili Ufanikiwe
Ukiharibu maisha ya mwingine, unaharibu ya
kwako! Unaweza kuita Karma, Gundu, au majina mengine, lakini jua ya kwamba hii
hutokea kweli. Pia ni ngumu kukaa na
hayo mafanikio Maana hutakuwa na plani ya pili ya mafanikio zaidi ya kudhurumu,
kuiba, kuua nk!
6.
Kuamini Wewe ni Mifupa na nyama tu!
Hili ni kosa kubwa sana maishani, wengi
huamini binadamu n mifupa na nyama tu, hivyo hakuna hata ya kufanya kazi kwa
bidii kwa kuwa tu “eti” Mwisho wa siku tutakufa na kuzikwa! Je, Unawaachia nini
wanao na kizazi chako? Je kwa nini hasa Mungu alitupa utashi tofauti na Mbuzi
na wanyama wengine?
Kumbuka, Tungeamua kuamini kuwa sisi ni Nyama na mifupa tu, kusingekuwa na Magari,
Simu, Majengo ya kisasa, na Hata hii dini tuliyonayo tusingeipata.
“do your part, make world a better place”
7.Kulaumu Vitu vinavyotokea na kutokuwa
tayari kutafuta suluhisho Pengine kwa kutotaka kufanya maamuzi magumu au
kutojua Majukumu yako ni yapi (badilika)
8. Kuamini kila kinachosemwa na “Wataalamu”
Siku
hizi kila sekta kuna watu wanaojiita wataalamu (mimi mmoja wapo!) Lakini
nasikitika kukuambia kuwa, wengi wa wataalamu hawa, hawako sahihi kwani siku
hizi watu wanapata kipato kutokana na kuyaelewa matatizo ya watu na si kujua
suluhisho.
Usimuamini mtu eti tu kwa kuwa analielezea
kwa uzuri na analielewa tatizo lako bali muamini anayeweza kutoa suluhisho
linalokuwa msaada kwa tatizo lako
9.
Kuhisi huwezi kwa kuwa kuna mtu anakuambia hivyo
Kuna watu maishani wapo sii tu kwa
kukukwamisha wewe, bali pia kumkwamisha kila anayewazunguka. Ukiona hakubaliki kwa jinsi ulivyo, basi jua huko
mahali sahihi. Usikubali kuishi kama mtu mwingine kwa kuwa tu unataka
kukubalika maishani.
10. Kuona huhitaji chochote cha kusoma
Maisha yanachekesha! Kitu kinaweza kuwepo
leo, na kesho kisikuwepo. Kama kuna kitu unataka kufanya, fanya sasahivi. Kama ni
wazo la muda mrefu, basi anza leo kutekeleza kidogo kidogo. Kila muda una
changamoto zake. Hata tajiri mkubwa duniani Bill gates anachangamoto zake
kulingana na nafasi aliyonayo.
Soma pia
kwa-mwenye-akili-timamu-lazima-ujiulize maswali haya kabla siku haijaisha
Soma pia
kwa-mwenye-akili-timamu-lazima-ujiulize maswali haya kabla siku haijaisha
asante sana mwandishi!
ReplyDeletemaneno kuntu.....ntambelea hii Blog Kila nipatapo nafasi, ubongo wangu uendelee kupata lishe bora+++++
ReplyDeletekaribu sana ndugu!
ReplyDeleteNiko happy sana
ReplyDelete