MADHARA 10 YA KUTUMIA SHISHA! (VIJANA WENGI HAWAJAYAJUI)
1.Kansa
Licha ya kupita ndani ya maji, moshi wa shisha huwa na
kiwango kikubwa cha carbon monoxide na nicotine ambazo humfanya mtumiaji awe
kwenye hatari kubwa ya Kupata Tatizo la kansa ya koo, ama mapafu.
2.Matatizo ya Moyo
Moshi na tumbaku husababisha mishipa ya damu ya artery Kuziba,
Matokeo yakemoyo hushindwa kufanya kazi kwa ufanisi wake.
3.Huharibu Fizi (periodontal disease)
Hii hutokana na kuongezeka kwa kiasi cha sumu ya nicotine
kwenye damu na fizi matokeo yake ni kuharibika kwa fizi na kupata matatizo ya
meno.
4. Fangasi na Kifua kikuu (TB)
Kutokana na kutosafishwa vizuri kwa bomba za kuvutia shisha
(hasa kutokana na wengi kujali kipato kuliko afya za watu) Mtumiaji hujiweka
kwenye hatari kubwa ya Kupata magonjwa ya kuambukizwa kama fangasi, au hata
vidonda vya tumbo kwa kuvuta kimelea cha helicobacteria
5.Kuzaa Njiti (mtoto mwenye uzito mdogo)
Hii ni kwa wanawake wanaotumia shisha wakiwa wajawazito. Pia
mtoto huyo ni rahisi kuwa na magonjwa yanayohusiana na upumuaji.
6. “Nicotine Addiction”
Hii ni hali ya kuwa mtumwa wa Sumu ya Nicotine. Mtumiaji wa
shisha huvuta kiwango sawa cha nicotine kama mvutaji wa sigara hii husababisha
sumu hii hatari kuingia kwenye damu yake, matokeo yake hataweza kuishi bila
kutumia shisha au sigara.
7.Kupoteza Uwezo za Kujamiiana.
Utafiti unaonesha kuwa, wanawake wanaotumia shisha hupoteza hamu ya kujamiiana kwa kiasi
kikubwa. Hali ni mbaya zaidi kwa wanaume kwani huchangia kwa kiasi kikubwa
upungufu wa nguvu za kiume.
8.Kuchakaa kwa ngozi.
Kama ilivyo kwa watumiaji wa sigara, matumizi ya shisha
huchangia kwa kiasi kikubwa katika uharibifu wa ngozi. Mtumiaji wa muda mrefu
wa shisha huzeeka haraka zaidi ya asiyetumia.
9.Asthma na Allergy Zingine
Uvutaji wa shisha huharibu utando laini uliopo kwenye njia
za pua na koo, uharibifu huu unaweza kusababisha matatizo ya allergy, na asthma.
10.Kwa kuwa Haina Ladha kama ya sigara, watu wengi (hasa
vijana) huona shisha ni mbadala mzuri wa sigara, bangi, na madawa mengine ya
kulevya wakihisi haina madhara kumbe wanajiangamiza wenyewe!
Doooo
ReplyDeleteElimu itolewe kwa vijana, wanazidi kuangamia
ReplyDeleteN vzur kama elmu ikgawiwa kwa vjana
ReplyDeleteIngekuwa vizuri kama walimu wa kutowa darasa ya kuhusu madhara ya shisha wangefunguliwa madarasa yao ili tuokoe nchi yetu
ReplyDeleteAisee
ReplyDeletesub hana llah mbna hii ya nguv za kiume na kukosa hamu kama inanichukua😭😭😭
ReplyDeleteWameilet na ladha mbalimbali ili tupende 🙆🙆🙆
ReplyDeleteHatari sana nimevuta siku moja sirudii tena.
ReplyDelete