UNA TATIZO LA KUCHELEWA KUAMKA? TUMIA NJIA HIZI KUMI KUWAHI KUAMKA ASUBUHI
1.Kuna chakula/tunda unalolipenda zaidi? Jiwekee zawadi,
kwamba ukiamka asubuhi tu cha kwanza ni kula
chakula hicho/ tunda/ chokleti nk. Hii itakufanya Utoke kitandani pale tu
atakaposhtuka!
2.Iwekee Kipaumbele kazi unayopenda kufanya zaidi iwe ya kwanza kutendeka asubuhi.
Utajkuta unatamani kuamka mapema zaidi kuwahi kazi hiyo na siku yako itaenda
vizuri
3.Andaa mapema nguo ya kuvaa siku inayofuatia, ili kuwahi
jumatatu, andaa nguo ya kuvaa jumapili usiku. Utafiti unaonyesha kuwa asilimia
40 (40%) ya watu huchelewa kutoka kitandani kwa kuwa walitumia muda mwingi
kupanga watavaa nguo gani.
4. Anza kupunguza dakika 20 kila siku Taratibu; Kama ulikua
unaamka saa mbili kamili, amka saa moja na dakika arobaini, baada ya siku mbili
punguza tena dakika ishirini mpaka utakaporidhika
5. Jiwekee Lengo na uwaambie watu. Hii itakufanya ufanye
kazi kwa bidii kwa kutaka kuwaonyesha watu kwamba umetimiza lengo lako na
utajikuta unawahi kuamka asubuhi
6. Tengeneza “appointment” (Miadi) ya kuonana na mtu
asubuhi, utajikuta unawahi kuamka kwa kuogopa kumuangusha mtu huyo.
7. Kama una mtu unaishi nae, tengeneza ratiba ya pamoja kama
kufanya mazoezi, maombi, kusoma nk! Itakusaidia kukuongeza morali ya Kuwahi
kuamka.
8 Weka saa ya kukuamsha (alarm clock) mbali na kitanda ikiwa na sauti kubwa, ni
vizuri ukitumia wimbo uupendao.
9. Muombe mpenzi wako akuamshe kila asubuhi, au jenga tabia
ya kumpigia mpenzi wako simu asubuhi
10.Ondoa vitu Vinavyokufanya uchelewe Kuamka mfano; pombe, kahawa na kuwahi kulala usiku.
Nzuri
ReplyDelete🤐
Delete