ULIYAJUA HAYA KUMI KUHUSU HARRIS KAPIGA MCHUNGAJI, MC, NA MTANGAZAJI WA CLOUDS FM?

ULIYAJUA HAYA KUMI KUHUSU HARRIS KAPIGA MCHUNGAJI, MC, NA MTANGAZAJI WA CLOUDS FM?

 1. Alishawahi kuishi nyumba isiyokuwa na choo, hivyo walikuwa wakienda kujisaidia kwa jirani.

2.Kila unachokiona leo kwa Harris, amekipata ndani ya miaka Kumi tu! Yaani mwaka 2004 (akiwa na miaka 29) hakuwa MC, mchungaji, nyumba, gari, mke, wala mtangazaji!

3. Kama Hujui Harris Kapiga Ndiye mchungaji aliyeanzisha klabu  ya usiku ya nyimbo za injili “Gospel club”


4. Ni Mtangazaji wa kituo cha redio cha clouds Fm, MC wa harusi, send off, kitchen party, matamasha nk, pia ni mchungaji wa kanisa la Nchi ya Ahadi lililoko sinza Kamanyola.

5.Hakufaulu kidato cha nne na hajawahi kusoma kidato cha tano na sita licha ya kuwa na Masters ya Maendeleo ya uchumi wa Jamii.

6.Akiwa darasa la nne aliambiwa na shemeji yake kwamba, kazi anayoiweza hapa duniani ni kuwa askari wa barabarani, au mchungaji. Hivyo asihangaike kusoma vitu vingine.

7.Hajawahi Kulazwa hospitalini hata mara moja.

8.Alishakosa Viza ya kwenda Marekani na UK mara Kumi!

9.HK anaamini kwamba, kila anachokitamani huwa anakipata japo kwa kuchelewa! Mfano mwaka 2000 alienda clouds fm kuomba kufanya kipindi cha gospel tracks hakukubaliwa, miaka kumi baadae alikubaliwa kufanya kipindi kilekile!

10. Harris amezaliwa wilaya ya Iramba mkoani singida tarehe 11 April 1975. ameoa, na ana watoto wawili.


8 comments:

  1. Aisee.kwanza nikupe hongera kaka Haris inaonekana wewe ni m2 usiyekata tamaa kabisa kwa sababu unamtegemea sana Mungu.una Imani kubwa.Hakika mkeo ni m2 wa bahati sana kumpata m2 kama wewe.MMEBARIKIWA

    ReplyDelete
  2. huyu jamaa fighter sana

    ReplyDelete
  3. what i always want to comment about u, is I SEE MYSELF IN YOU.WISHING U A PROSPEROUS LIFE WITH UR FAMILY.

    ReplyDelete
  4. Kwa kweli Ni kijana anayefaa kuigwa kwa kutokukata tamaa Ni ushindi mkubwa Sana

    ReplyDelete

Toa maoni yako

Copyright © 2014 Kumi Muhimu