MAMBO KUMI YA KUZINGATIA UNAPOTAKA KUACHA POMBE
1.Kama ni mlevi uliyebobea na
unahisi huwezikuacha kwa siku moja, anza kwa kupunguza kiwango cha kunywa,
yaani kama unakunywa bia tatu kwa siku, anza kunywa moja, baadae moja kwa siku
mbili mpaka utakapozoea kuishi bila pombe.
2.Epuka
kuweka kilevi au pombe nyumbani au sehemu ya kazi ili kuepuka majaribu.
3.Usipende
kuruka mlo, kula chakula mara 3 mpaka nne (4) kwa siku ili kuupatia mwili virutubisho
vyote muhimu.
4.Ondoa dhamira potofu kwamba huwezi kuishi pasipo kunywa pombe. Kumbuka mwili
wako umeumbwa kikamilifu kukabili hali zote za Maisha hivyo usihisi kuwa pombe
ndio kichocheo chako kila unapotaka
kufanya jambo Fulani.
5.Zingatia
mlo kamili, na jifunze kula matunda kwa wingi.
6.Anza
kufanya mazoezi na upange ratiba hii muda ambao ulikuwa ukitumia kunywa pombe.
7.Kumbuka
mambo mabaya ambayo yalikutokea kutokana na pombe katika maisha yako. Hii itakusaidia
kutothubutu tena kunywa pombe.
8.Ongeza
unywaji wa maji jenga mazoea ya kunywa angalau glasi tano (5) za maji kwa siku.
9.Jenga
mazingira ya kujizawadia kutokana na uamuzi wako mzuri wa kutokunywa pombe.
10.Washirikishe
ndugu, jamaa na mrafiki wa karibu kuhusu uamuzi wako wa kuacha pombe na pia
usijione mjinga kwa wale watakao kucheka.
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako