USILIKATIE TAMAA JAMBO ULILOPIGANIA KWA MUDA MREFU FUATA HATUA HIZI KUMI KULIKAMILISHA.
1.Kaa
chini na uangalie lengo hasa la wewe
kulianza jambo hilo. Zikumbuke sababu ulizojiwekea mwanzoni kwamba ni kwanini
unataka lengo lako litimie. Itakufanya ujione mpya na uhisi kwamba ndio kwanza
unalianza!
2. Kabla
hujakata tama jiulize ni kwa nini ulianza? Na ni kwanini umelipigania kwa muda
wote huo?
3.Andika
vitu vyote vizuri utakavyovipata ukishalimaliza jambo hilo, Vipitie kila mara
unapotaka kufanya jambo hilo.
4.Elewa
kwamba, Vikwazo na changamoto ni Muhimu wakati mwingine! Kikubwa ni kujipa
moyo, kuboresha mipango yako kulingana na muda na mabadiliko ya dunia, na la Muhimu
zaidi ni kujifunza kutokana na vikwazo na changamoto ulizozipata!
5.Tafakari
ni kipi unakiweza zaidi? Kitilie mkazo na usijali unakosea kiasi gani bali fikiria
umepiga hatua gani!
6.Punguza
Vitu Kichwani hasa vile usivyovihitaji zaidi. Pia punguza idadi ya marafiki
wasiokuwa na msaada kwako ambao wengi wao hawatakupa msaada wowote zaidi ya
kuangalia unakosea wapi.
7.Kuwa
na muda wa kupumzika, fanya matembezi,na kulala usingizi wa kutosha.
8.Tambua
kuwa hauko peke yako! Hili pengine ndilo zuri kuliko yote.. Hakuna aliyefanikiwa bila kupitia kipindi Fulani
kigumu ambacho pengine kilimfanya afikirie kukata tama! Never Give up.
9.Kumbuka,
Ukijaribu njia kumi ukashindwa kufika unapokwenda, ukaweza mara ya kumi na moja,
hujapoteza kitu Bali umegundua njia kumi zisizofanikisha! Hivyo wakati mwingine
hutapitia njia hizo.
10.Soma
Vitabu au historia ya watu waliofanikiwa duniani uone wamepitia magumu mangapi!
Pia unaweza kutafuta mshauri (Mentor).
2. Kabla hujakata tama jiulize ni kwa nini ulianza? Na ni kwanini umelipigania kwa muda wote huo?
3.Andika vitu vyote vizuri utakavyovipata ukishalimaliza jambo hilo, Vipitie kila mara unapotaka kufanya jambo hilo.
5.Tafakari ni kipi unakiweza zaidi? Kitilie mkazo na usijali unakosea kiasi gani bali fikiria umepiga hatua gani!
6.Punguza Vitu Kichwani hasa vile usivyovihitaji zaidi. Pia punguza idadi ya marafiki wasiokuwa na msaada kwako ambao wengi wao hawatakupa msaada wowote zaidi ya kuangalia unakosea wapi.
7.Kuwa na muda wa kupumzika, fanya matembezi,na kulala usingizi wa kutosha.
8.Tambua kuwa hauko peke yako! Hili pengine ndilo zuri kuliko yote.. Hakuna aliyefanikiwa bila kupitia kipindi Fulani kigumu ambacho pengine kilimfanya afikirie kukata tama! Never Give up.
9.Kumbuka, Ukijaribu njia kumi ukashindwa kufika unapokwenda, ukaweza mara ya kumi na moja, hujapoteza kitu Bali umegundua njia kumi zisizofanikisha! Hivyo wakati mwingine hutapitia njia hizo.
10.Soma Vitabu au historia ya watu waliofanikiwa duniani uone wamepitia magumu mangapi! Pia unaweza kutafuta mshauri (Mentor).
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako