NJIA KUMI ZA HARAKA KUONDOA “STRESS” NA UCHOVU
1.Pitia picha zako zako za zamani kidogo, Picha za tukio moja wapo lililokufurahisha au
za mtu mwingine yeyote wa karibu yako!
2.Fungua madirisha na kuruhusu mwanga na hewa kupita kwa
kiasi kikubwa. Epuka kukaa sehemu yenye mwanga mdogo kwani hufanya hali yako ya
uchovu au stress kuwa juu zaidi.
3. Imba huku unaoga! Sio lazima uwe muimbaji mahiri bali
chagua tu wimbo wako unaoupenda, imba kwa namna yeyote huku ukiendelea kuoga
4. Epuka kubaki mpweke. Tafuta mtu yeyote uongee nae (hata
mtoto mdogo) itakusaidia kupunguza mawazo au uchovu
5. Sikiliza muziki au mpigie simu rafiki yako mliyepotezana
muda mrefu.
6. Fanya Mazoezi (japo kwa dakika moja)
7.Badilisha Mazingira, Mfano kama unapita njia hiyohiyo moja
kutoka kazini/shule, badilisha na upite nyingine.
8. Fanya utafiti wa kijinga kwa kuwaangalia wapita njia na
kutoa kasoro zao kimavazi, muonekano wao bila ya wao kujua.
9. Nenda Saluni kunyoa/kuosha/kusuka nywele zako.
10. Chukua kalamu na karatasi, anza kujifunza kuchora!
Soma pia
Unahitaji kucheka?>>Lazima-huwa-unafanya-moja-ya-vitu-hivi. unapohisi huonwi na mtu<<
Una stress?>> Soma-tafiti-hizi-kumi-kuhusu siku ya j'tatu ubaki mdomo wazi<<
hupati usingizi?>> unene-na-matatizo-mengine-10 yanayoletwa na kukosa usingizi wa kutosha<<
hupati usingizi?>> unene-na-matatizo-mengine-10 yanayoletwa na kukosa usingizi wa kutosha<<
Gud
ReplyDeleteSafi Sana nimekuelewa
ReplyDelete