UMEBOREKA? SOMA TAFITI HIZI KUMI KUHUSU SIKU YA JUMATATU UBAKI MDOMO WAZI!
Nasikia kitu kibaya zaidi siku ya jumapili ni pale tu
unapowaza kesho ni jumatatu tena na unavitu kibao vinakungoja! Haya ni mambo
kumi yatakayokuacha mdomo wazi kuhusiana na siku ya jumatatu.
1.Kwa siku ya jumatatu, Asilimia 60 ya watu hupata tabasamu
lao la kwanza saa tano asubuhi (Kabla ya hapo kila mtu huwa amenuna!)
2. Asilimia 50 ya wafanyakazi huchelewa kazini siku ya
jumatatu kwa kisingizio cha foleni. Pia ndio siku inayoongoza kwa “sicksheet”
nyingi zaidi katika wiki.
3.Kwa kiasi kikubwa saa zima la kwanza kazini huwa kazi
haziendelei kila mtu hukuuliza weekend ilienda vipi na kuishia kuzungumzia
yaliyotokea hapo kabla, na kazi hufanyika kwa masaa machache zaidi kuliko siku
zingine
4. watu wenye umri wa miaka 35 mpaka 50 wako kwenye hatari
kubwa sana kupata matatizo ya moyo ikiwemo kiharusi siku za Jumatatu!
5. Kwa mujibu wa wataalamu wa saikolojia, Watu wengi zaidi
hujiua siku ya jumatatu kuliko siku nyingine yeyote katika juma
6. Siku hii ya jumatatu, ndio siku inayoripotiwa kupata nvua
kidogo zaidi kuliko siku nyingine! Wengi huamini hili linatokana na uharibifu
wa hali ya hewa unaofanyika mwishoni mwa wiki!
7.Licha ya kuchukiwa na watu wengi, jumatatu ndio siku bora
zaidi kununua gari na bidhaa zingine! Hii ni kwa kuwa wauzaji wengi huwa
wametumia kiasi kikubwa cha fedha wikendi na jumatatu huwa na wateja wachache
zaidi hivyo ni rahisi kupunguziwa bei!
8.Kuamka siku za jumatatu huwa kitu kigumu zaidi kukumbana
nacho, usingizi huongezeka kadri muda wa kazi unavyokaribia
9. Kazi ulizoacha kiporo siku ya ijumaa huonekana ngumu
zaidi ya kawaida na shinikizo kutoka kwa wakubwa zako huongezeka!
10. Jinsi ya kuepuka
haya, lala mapema siku ya j’pili, andaa nguo utakayoivaa mapema, andaa vitu
utakavyobeba mapema, weka malengo kadhaa ya kutimiza siku ya jumatatu!
Soma pia
Ulishawahi-kukutana-na-nyakati-hizi.za Kuudhi?
aina-ya-watu-na-vitu-10-vinavyoudhi.zaidi maofisini
Soma pia
Ulishawahi-kukutana-na-nyakati-hizi.za Kuudhi?
aina-ya-watu-na-vitu-10-vinavyoudhi.zaidi maofisini
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako