UNENE NA MATATIZO MENGINE 10 YANAYOTOKANA NA KUKOSA USINGIZI WA KUTOSHA

UNENE NA MATATIZO MENGINE 10 YANAYOTOKANA NA KUKOSA USINGIZI WA KUTOSHA

1.Hupunguza uwezo wako wa kujifunza .
Kukosa usingizi hupunguza umakini na uwezo wa kupokea habari kwenye ubongo wako na kukuwia vigumu kujifunza mambo mapya.

2.Kuchanganyikiwa, na mtu huwa mwepesi Kukasirika.
kutokana na kupunguza ule uwezo wa ubongo kufikiria nan a kukabili hali mbalimbali za mwili kama hasira, mshtuko nk

3.Huongeza Kusahau na kupunguza uwezo wa kufanya maamuzi


4.Kuongezeka uzito kwa haraka
Utashangaa lakini ukweli ni kwamba  kukosa usingizi huufanya mwili utengeneze kwa wingi homoni ya ghrelin inayohusika na kukufanya ujisikie njaa. Hivyo mtu anaekosa usingizi wa kutosha hula chakula kingi bila kutosheka na kuongeza uwezekano wa kuongezeka uzito
5. Kuharibika kwa ngozi yako.
Kukosa usingizi kwa siku moja tu hufanya ngozi ya mtu kufubaa hasa za chini ya macho. Na ukiendelea tatizo hili huwa ni la kudumu.
6. Magonjwa kama kiharusi “stroke”,  Shinikizo la damu, kisukari ni rahisi kumpata ntu anekosa usingizi wa kutosha kuliko mtu anaepata usingizi wa kutosha.
7. Hupunguza Uwezo wa Kujamiiana
Ukosefu wa usingizi  hupunguza hamu ya kufanya mapenzi kwa wanaume na wanawake pia. Hii hutokana na muda Mwingi kuwa wamechoka. Kwa wanaume kukosa usingizi, hushusha uzalishaji wa homoni za “testosterone” na kupunguza nguvu za kiume.
8.Ajali (kutokana na kukosa umakini)

9. Hupunguza uwezo wako wako wa kinga mwilini.
 Usingizi huchukua nafasi kubwa sana kuongeza kinga yako ya mwili na kuzuia magonjwa madogo madogo  hasa ya msimu kama mafua, kikohozi nk.

10.Hupunguza uwezo wako wa kawaida wa kuona na kuzeeka haraka.

Soma pia

0 comments:

Post a Comment

Toa maoni yako

Copyright © 2014 Kumi Muhimu