REKODI KUMI ZA KIJINGA ZAIDI ZILIZOPO KWENYE KITABU CHA REKODI CHA “GUINNESS”

REKODI KUMI ZA KIJINGA ZAIDI ZILIZOPO KWENYE KITABU CHA REKODI CHA “GUINNESS”

1.Vijiko Vingi zaidi kwenye mwili wa Binadamu.
Disemba 28 mwaka 2013, Etibar Elchiyev aliweka vijiko 53 mwilini mwake akiwa amesimama wima na kuvunja rekodi yake mwenyewe!












2.Mtu aliyeolewa mara nyingi zaidi!
Linda Lou Taylor wa jimbo la  Indiana nchini marekani, anashikilia rekodi ya kuolewa mara nyingi zaidi akiwa ameolewa mara  23!. Ana miaka 69 kwa sasa na amekuwa akisisitiza kutaka kuolewa kwani hana mpenzi  kwa zaidi ya miaka kumi sasa!








3.Watu wengi zaidi Kupiga Mswaki kwa wakati mmoja.
Katika mji wa Manila Nchini Philippines, wanafunzi  10,800 walikusanyika pamoja kupiga mswaki na kutema kwenye kikombe kwa wakati mmoja!











4.Mbwa aliyebeba glass na kutembea umbali Mrefu zaidi.
Usishangae! Wanyama nao wamo. Mmbwa mmoja wa Australia anashikilia rekodi ya kutembea hatua kumi mbele na hatua  kumi nyuma  akiwa na glass ya maji kichwani!









5.Nywele Ndefu zaidi za Masikioni.
Agosti 26 mwaka  2007, Anthony Victor wa Maduri India, aliweka rekodi ya dunia kuwa binadamu mwenye nywele ndefu zaidi za masikioni zikiwa zimefikia nchi 7!









6.Kupigwa Teke Sehemu za siri (mwanaume) kwa spidi ya kilometa 40 kwa saa.
Kirby Roy aliweka rekodi hii alipokubali kupigwa teke zito na mwanamieleka Justice Smith kwa kasi ya kilometa 40 kwa saa teke hilo likiwa na nguvu ya kusogeza kilo mia tano!












7. Choo chenye Kasi zaidi Duniani
Unapoteza muda mwingi  kukaa chooni? Colin Furze alitengeneza choo cha kukaa chenye uwezo wa kutembea kwa kasi ya kilometa 100 kwa saa chenye uwezo wa kuflashi!






8.Kuongezeka Uzito kwa kasi zaidi.
Rekodi hii imewekwa na Donna Simpson wa  New Jersey, USA.  Alifikisha kilo 273.5 kutoka kilo tisini tu! Zoezi hilo alilifanya kwa kipindi cha miaka miwili (2) tu! Alikuwa akitumia zaidi ya shilingi milioni moja kwa wiki kwa kula tu!








9.Mayai Mengi zaidi kupasuliwa kwa kichwa kwa wakati mmoja.
 Ashrita Furman anashikilia rekodi ya kupasua mayai  80 kwa kichwa kwa wakati mmoja!










10.Chapati Kubwa Zaidi kutengenezwa!

October 8 2010, katika nchi ya Uturuki, wapishi zaidi ya 50 walikusanyika kwa pamoja na kutengeneza chapatti ya mayai yenye uzito wa tani 6 (Uzito wa gari kubwa). Chapatti hiyo ilichanganywa mafuta lita mia nne (400), na Mayai zaidi ya laki moja (100,000)

1 comment:

  1. Nimependa ya choo Cha kutembea hakika hii ni rekodi za kijinga🤣✍️🙏

    ReplyDelete

Toa maoni yako

Copyright © 2014 Kumi Muhimu