UNATAKA KUMILIKI BLOG? USIKURUPUKE, YAJUE HAYA KUMI KWANZA
Natakiwa nifungue blog wapi? Nianzishe blog inayohusu nini?
Lazima niandike kuhusu Diamond na Wema? Ntawezaje kuingiza kipato? Nimaswali
ambayo wengi hujiuliza kabla ya kuamua kuwa na blog. Kama
Ulikuwa hujui, Kuna Blog zaidi ya milioni 150 Dunia nzima! Bila kujali unataka kuanzisha kwa madhumuni
yapi, zingatia haya kumi.
1.Unaweza kufungua blog bure kupitia sehemu mbalimbali lakini
watu wengi hutumia blogspot (jinalako.blogspot.com) au wordpress (jinalako.wordpress.com).
Kwa sasa Blogspot ni maarufu zaidi kuliko wordpress kwa kuwa blogspot ni mali
ya google. Hivyo kama unataka blog yako ipatikane kwa haraka basi tumia
blogspot. Kwa upande wa Wordpress, inavutia zaidi, usalama na pia ni rahisi
zaidi kuhamia .com
2. Blog Hukatisha sana tama miezi sita ya Mwanzo! Na wengi
huishia kipindi hiki na kuhisi haiwezi kumlipa na kuamua kuitelekeza.
3. Andika angalau kitu kimoja kila siku. Muda Mzuri wa
kuandika ni asubuhi. Usiandike post fupi sana kwani watu wataidharau na
hawatarudi tena.
4.Unganisha blog yako na Mitandao ya kijamaa ili kuwafikia
watu wengi zaidi. Unaweza kutumia app kama “Networked blogs” au “Twitterfeed”
zitakusaidia kusambaza post zako kwenye mitandao hiyo ya kijamii.
5.Picha na Kichwa cha habari yako kiendane na ulichoandika
kwenye post yako. Vinginevyo utapata
watu wengi kwa wakati mmoja, na hakuna atakaerudi kwako tena kwani hakupata
alichokifuata. Haina faida kupata watu elfu kumi leo, halafu kesho usipoandika
chochote unapata watu watano!
6. Blog za habari na udaku ndizo zenye wafuatiliaji wengi
zaidi hasa kwa nchi yetu, Hivyo kama unaamua kufungua blog ya habari au udaku,
hakikisha una watu wanaokutafutia habari kona zote, usitegemee kunakiri kwa mtu
mwingine kila siku kwani utajikuta unaonekana wewe ni mfuasi wa wenzio na si
mshindani.
7.Usikimbilie kuweka Matangazo ua “adsense” au “adwords” kwani huwaudhi watembeleaji na blog yako haitakuwa
na mashabiki na hivyo, haitadumu muda mrefu. Weka Matangazo haya baada ya kukua
vyakutosha na unauhakika wa kundi kubwa nyuma yako.
8.Usiweke Pesa mbele, hakikisha kwanza blog yako inataarifa
za kutosha kuhusu unachokiandika, Itakulipa baadae sana baada ya kuaminiwa na
watu. Ukitaka fedha nyingi kutoka kwenye blog, hakikisha unawekeza kwenye blog hiyo kwa kuitangaza.
9. Wafanye watu wazunguke kwenye blog yako kwa kuweka post
zingine zinazofanana na hiyo uliyoweka pembeni yake (Related posts/ recommended
posts)
10.Linalobeba yote katika suala la kuamua kuwa na blog ni
neno UVUMILIVU. Kwanza utaonekana umekosa cha kufanya, kuna kipindi watu
hawatakuunga mkono kabisa, baadae unaweza kukata tama baada ya kuona kiasi cha
ushindani ni kikubwa sana! Unatakiwa usiwe na haraka, jaribu kutengeneza blog
leo, hakikisha unakuwa na kiyu kipya kila siku bila kukata tamaa kwa mwaka mzima
bila kujali unapata watu wangapi, baadae itakulipa tu! Usiwe na shaka..
sawa kaka nimekuelewa mana mimi nilishakata tamaa
ReplyDeleteNatamani Sana niwe na blog
ReplyDeleteTutembelee tukuudumie 0625539736
DeleteNatamanisana nijue kutengeneza Blog
ReplyDeleteSawa kaka ngoja tupambane
ReplyDeleteSwafi saaana kaka
ReplyDeleteSure
ReplyDeleteMimi pia ninablog ila sifahamu namna itakavyonilipa je waweza nisaidia
ReplyDeleteAsante kwa kwa maelekezo mazuri mwl. Swali naanzia wapi kuanza kufungua blog
ReplyDeleteTueleze namna ya kutengeneza tovuti
ReplyDeleteUTAJIRI AU FEDHA ZA NDAGU AU MAJINI KWA MUDA MFUPI
ReplyDelete(Kwanza kabisa nataka kukwambia kwamba hakika utajili ni azina kutoka kwa mwenyezi mungu na pia kuna viumbe alio wapa mamlaka na nguvu ya kumiliki mali)
MPAKA MASAA 72(SIKU3) PAPO HAPO KWA MASHARTI MAALUM KIKUBWA UWE MWAMINIFU, JASILI NA UWE NA UTAYARI WA KUPOKEA MASHARTI YA KUTUNZA SIRI HII SIO MZAHA......
KUMBUKA MALIPO NI BAADA YA KUFANIKIWA
kwa maelezo kamili piga namba +255742162843
(KWANINI USUMBUKE,HACHA KUTANGATANGA, NA MAISHA NI MAFUPI PUUZA UONGOFU WA KUWA MTU KUWA TAJIRI NI DHAMBI WAKATI AKUAMBIAE YEYE NI TAJIRI (Tumia ufahamu kujinasuaUTAJIRI WA NDAGU(MASHARTI) NDANI YA MASAA 72(SIKU TATU) PAPO HAPO KIKUBWA UWE MWAMINIFU, JASILI NA UWE NA UTAYARI WA KUPOKEA MASHARTI YA KUTUNZA SIRI HII SIO MZAHA......
NAITWA DR, MDIRO piga 0742162843. KAMA UNAITAJI PESA ZA MAJINI AU NDAGU YA MALI AU ULINZI KWA MALI YAKO
(HUSITUME SMS PIGA SIMU KUHEPUKA MATAPELI)
MATIBABU MENGINEYO NI KAMA UTULIVU KATIKA NDOA, AU KUMVUTA UMPENDAE, KUONDOA MIKOSI, MABALAA, KUOSHA NYOTA, KUITAMBUA NYOTA YAKO NA ASILI YA KAZI YAKE, KAMA UNASUMBULIWA NA MAJINI MAHABA NA SHIDA YA UZAZI.
NIPIGIE 0742162843. KIKUBWA NI KUSIKILIZA NA KUFATA MASHARTI. ANGALIZO USITUME SMS PIGA NA UWE NA NIA.
(kuhusu utajiri au pesa) KABLA YA KUPIGA SIMU ZINGATIA YAFUATAYO
1. uwe una umri wa miaka 18+
2. uwe tayari kupokea masharti yote
3.uwe na uwezo wa kutunza siri
4. uwe jasiri wa kupokea taarifa yoyote
KARIBU SANA KWA SHIDA NYINGINE PIA ULIYONAYO