UGONJWA WA EBOLA- YAJUE HAYA KUMI KUHUSU UGONJWA HUU HATARI.
1.Dalili za kwanza za ebola hufanana sana na dalili nyingine
za magonjwa yanayosababishwa na virusi kama kuumwa kicha, viungo, maumivu ya
tumbo, kuhara na kutapika hivyo mgonjwa anaweza kuhisi ana tatizo jingine mpaka
dalili za baadae zinapojionyesha.
2.Kutokwa damu ni dalili ya baadae sana wakati ugonjwa
umeshasambaa vya kutosha mwilini . Usidharau dalili za kwanza hasa kama unahisi
umegusana na mgeni yeyote kutoka maeneo yaliyo na maambukizi ya Ebola.
3. Mlipuko mkubwa zaidi wa ebola ulikuwa mwaka 1995 ambapo
watu 315 waliumwa ugonjwa huo, na watu
244 walipoteza maisha nchini Zaire (DRC)
4. Virusi vya ebola
huzaliana kwa kasi sana. Ndani ya masaa nane, mamilioni ya virusi huzaliana na
kusambaa kwa kasi mwilini.
5.Mtu wa kwanza kuumwa ugonjwa wa ebola alikuwa akiishi Zaire pembezoni mwa mto Ebola mnamo mwaka
1976. Nchi zingine zilizowahi kupata mlipuko wa ebola ni Sudan ya kusini,
Uganda, Gabon na Guinea kwa Nyakati tofauti.
6.Dalili nyingi za Ebola huanza kuonekana siku 10 mpaka 20
toka mtu apate maambukizi ya ugonjwa huu.
7. Tofauti na miaka mingine, mwaka huu Ebola Imeenea maeneo
ya Mjini zaidi na si vijijini kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.
8.Ebola Huua asilimia 90 ya watu wanaoupata ugonjwa wa
ebola. Mgonjwa hupata Maumivu makali sana mwili wote na hufariki siku chache
baada ya kuanza kutoa damu sehemu za wazi.
9. Mpaka sasa ni nchi nne za Afrika magharibi
zilizothibishwa kusambaa kwa ebola. Guinea, Sierra-Leone, Liberia, na Nigeria.
10. Mpaka sasa, Dawa na Kinga ya Ebola havijapatikana japo
kuwa Utengenezwaji unaendelea na kufanyiwa utafiti.
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako