HATUA KUMI ZA KUFUATA (Pamoja na Picha) UNAPOFUNGUA CHUPA YA SHAMPENI (Champagne)
1.Kabla ya
kuanza kufungua, hakikisha chupa yenye
shampeni imehifadhiwa kwenye ubaridi kwa muda Fulani kwani kinywaji hiki ni
bora zaidi kikinywewa kikiwa baridi. Unaweza usiweke kwenye baridi kama tu
unataka shampeni iruke sana na kusambaa kila mahali.
2.Itoe
Shampeni kwenye Jokofu au mahali popote ulipoihifadhi, Futa chupa na kitambaa
lain (kisafi) Kuzuia Kuteleza mikononi mwako.
3. Ondoa
Karatati inayozunguka shingo na mdomo wa chupa ya shampeni. Ili kuondoa
Karatasi hiyo, zungusha chupa yako na kutazama kiungio cha karatasi hiyo na
kuivuta taratibu.
4.Utaona
waya uliosukwa kuzunguka kizibo cha
chupa ya shampeni. Waya huo unazuia kizibo hicho kisitoke kunapokuwa na presha kubwa,
joto, au mtikisiko.
5.Weka kidole
gumba cha mkono uliotumia kushika shingo ya chupa ya shampeni, tumia mkono wako mwingine kuondoa waya unaozunguka kifuniko cha chupa.
Kumbuka waya
huo huondolewa kwa kuzungusha ukianzia sehemu ya pembeni iliyofungwa kama
kitanzi.
6.Ondoa
waya na kuuweka pembeni. Bila kuachia kizibo, Unaweza Kutikisa chupa mara kadhaa kama unataka shampeni iruke. Kama
hutaki iruke basi usitikise chupa hiyo.
7. Weka
kitako cha chupa Tumboni kwako ili kuipa balance huku mdomo wa chupa ukiangalia
juu kwa nyuzi 45 (45 degrees). Hii itazuia kizibo au shampeni kumrukia mtu
aliyeko karibu wala wewe.
8.Achia
Kidole kilicho juu ya kizibo, Huku mkono wako mmoja ukiwa umeshika shingo ya
chupa (usiielekeze chupa kwa mtu) na mwingine ukiwa huru.
9. Anza
kuzungusha kizibo cha chupa taratibu kulia na kushoto huku ukikivuta taratibu
sana mpaka kitoke. Kumbuka unaweza kukiachia kiruke au kukishikilia kama ni
tafrija inayohitaji utulivu sana.
10.Hongera, umeshajua Kufungua Shampeni. Nyanyua chupa juu, na kuanza kugawa kwa watu.
1.Kabla ya kuanza kufungua, hakikisha chupa yenye shampeni imehifadhiwa kwenye ubaridi kwa muda Fulani kwani kinywaji hiki ni bora zaidi kikinywewa kikiwa baridi. Unaweza usiweke kwenye baridi kama tu unataka shampeni iruke sana na kusambaa kila mahali.
4.Utaona waya uliosukwa kuzunguka kizibo cha chupa ya shampeni. Waya huo unazuia kizibo hicho kisitoke kunapokuwa na presha kubwa, joto, au mtikisiko.
5.Weka kidole gumba cha mkono uliotumia kushika shingo ya chupa ya shampeni, tumia mkono wako mwingine kuondoa waya unaozunguka kifuniko cha chupa.
8.Achia Kidole kilicho juu ya kizibo, Huku mkono wako mmoja ukiwa umeshika shingo ya chupa (usiielekeze chupa kwa mtu) na mwingine ukiwa huru.
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako