UNATAKA KUMILIKI BLOG? USIKURUPUKE, YAJUE HAYA KUMI KWANZA

UNATAKA KUMILIKI BLOG? USIKURUPUKE, YAJUE HAYA KUMI KWANZA

Natakiwa nifungue blog wapi? Nianzishe blog inayohusu nini? Lazima niandike kuhusu Diamond na Wema? Ntawezaje kuingiza kipato? Nimaswali ambayo wengi hujiuliza kabla ya kuamua kuwa na blog.   Kama Ulikuwa hujui, Kuna Blog zaidi ya milioni 150 Dunia nzima!  Bila kujali unataka kuanzisha kwa madhumuni yapi, zingatia haya kumi.

1.Unaweza kufungua blog bure kupitia sehemu mbalimbali lakini watu wengi hutumia blogspot (jinalako.blogspot.com) au wordpress (jinalako.wordpress.com). Kwa sasa Blogspot ni maarufu zaidi kuliko wordpress kwa kuwa blogspot ni mali ya google. Hivyo kama unataka blog yako ipatikane kwa haraka basi tumia blogspot. Kwa upande wa Wordpress, inavutia zaidi, usalama na pia ni rahisi zaidi kuhamia .com


2. Blog Hukatisha sana tama miezi sita ya Mwanzo! Na wengi huishia kipindi hiki na kuhisi haiwezi kumlipa na kuamua kuitelekeza.

3. Andika angalau kitu kimoja kila siku. Muda Mzuri wa kuandika ni asubuhi. Usiandike post fupi sana kwani watu wataidharau na hawatarudi tena.

4.Unganisha blog yako na Mitandao ya kijamaa ili kuwafikia watu wengi zaidi. Unaweza kutumia app kama “Networked blogs” au “Twitterfeed” zitakusaidia kusambaza post zako kwenye mitandao hiyo ya kijamii.

5.Picha na Kichwa cha habari yako kiendane na ulichoandika kwenye post yako.  Vinginevyo utapata watu wengi kwa wakati mmoja, na hakuna atakaerudi kwako tena kwani hakupata alichokifuata. Haina faida kupata watu elfu kumi leo, halafu kesho usipoandika chochote unapata watu watano!

6. Blog za habari na udaku ndizo zenye wafuatiliaji wengi zaidi hasa kwa nchi yetu, Hivyo kama unaamua kufungua blog ya habari au udaku, hakikisha una watu wanaokutafutia habari kona zote, usitegemee kunakiri kwa mtu mwingine kila siku kwani utajikuta unaonekana wewe ni mfuasi wa wenzio na si mshindani.

7.Usikimbilie kuweka Matangazo ua “adsense” au  “adwords” kwani  huwaudhi watembeleaji na blog yako haitakuwa na mashabiki na hivyo, haitadumu muda mrefu. Weka Matangazo haya baada ya kukua vyakutosha na unauhakika wa kundi kubwa nyuma yako.

8.Usiweke Pesa mbele, hakikisha kwanza blog yako inataarifa za kutosha kuhusu unachokiandika, Itakulipa baadae sana baada ya kuaminiwa na watu. Ukitaka fedha nyingi kutoka kwenye blog, hakikisha  unawekeza kwenye blog hiyo kwa kuitangaza.

9. Wafanye watu wazunguke kwenye blog yako kwa kuweka post zingine zinazofanana na hiyo uliyoweka pembeni yake (Related posts/ recommended posts)


10.Linalobeba yote katika suala la kuamua kuwa na blog ni neno UVUMILIVU. Kwanza utaonekana umekosa cha kufanya, kuna kipindi watu hawatakuunga mkono kabisa, baadae unaweza kukata tama baada ya kuona kiasi cha ushindani ni kikubwa sana! Unatakiwa usiwe na haraka, jaribu kutengeneza blog leo, hakikisha unakuwa na kiyu kipya kila siku bila kukata tamaa kwa mwaka mzima bila kujali unapata watu wangapi, baadae itakulipa tu! Usiwe na shaka..

10 comments:

Toa maoni yako

Copyright © 2014 Kumi Muhimu