TABIA KUMI(10) MBAYA ZA WATU WANAOISHI PEKE YAO NYUMBANI. SOMA UCHEKE

TABIA KUMI(10) MBAYA ZA WATU WANAOISHI PEKE YAO NYUMBANI. SOMA UCHEKE

1.Huacha Mapambo, au vitu vilivyotumiaka katika sherehe iliyokuwa miezi kadhaa iliyopita kama sikukuu ya kuzaliwa, mti wa chrismass mapambo ya ukutani ya mwaka mpya nk.

2. Kutumia Miguu kwenye shughuli zinazotakiuwa utumie mikono kama kubonyeza swichi, kusogeza vitu, kufunga mlango nk.

3.Kuacha vyombo vichafu mpaka vinaota utando, au kutumia vyombo vichafu.

4.kutumia meza ya chakula kwa shughuli zingine zote kasoro kulia chakula! Mfano, kuweka nguo, rimoti za tv, vifaa vibovu, au vyombo vichafu nk.

5.Kubadili kitanda kuwa begi la nguo, na vifaa vya kazi, huweka nguo pembeni anapolala, na kuzirudisha kitandani akiamka.

6. Hunywa vinywaji moja kwa moja kwenye mdomo wa chupa bila kutumia glass wala vikombe. Na akipika, basi atakula kwa kutumia chombo hiucho hicho alichopikia.

7.Kutopenda kupika na kula mkate au matunda yote yaliyohifadhiwa kwa wakati mmoja. Wakati mwingine hununua vyakula vingi kupita kiasi na kuacha viharibike bila kupiuka wala kuvitumia.

8. Kucheza michezo ya kitoto ndani, na mara nyingi kuwa mchafu kupitiliza.

9.Kutojali kutengeneza  vitu vilivyoharibika kwa wakati.

10. Hawapendi wageni wanaokuja bila taarifa kwani wengi wanachojali ni nguo zao tu, kwa kuwa  ndizo zitakazoonekana wanapotoka!

0 comments:

Post a Comment

Toa maoni yako

Copyright © 2014 Kumi Muhimu