UNATATIZO LA KUSAHAU SANA? TUMIA NJIA HIZI KUMI KUBORESHA KUMBUKUMBU YAKO!

UNATATIZO LA KUSAHAU SANA? TUMIA NJIA HIZI KUMI KUBORESHA KUMBUKUMBU YAKO!

1. Jifunze kufanya kazi moja kwa wakati mmoja. Kama unajifunza kitu basi jifunze kitu kimoja kwa wakati/siku moja. Hii itaepusha kuchanganya mambo utakapokuwa unakumbuka

2.Tafuna  Bazoka (chewing gum) unapofanya kazi inayohitaji kumbukumbu kubwa au unaposoma kitu kipya. Kwa mujibu wa wataalamu wa mambo ya saikolojia, utafunaji wa bazoka hufanya misuli ya kichwa kuwa “active” .


3. Fanya mazoezi ya viungo kama kukimbia, pushup, kuendesha baiskeli nk!

4.Kunja ngumi  unapojifunza au kukumbuka jambo! Hii inaweza kukuchekesha na ikawa rahisi sana lakini utafiti unaonesha kuwa, watu wanaokunja mmoja wa mikono yao wanapojifunza/kusoma, huwa na kumbukumbu zaidi ya wasiokunja ngumi.

5.Punguza kiasi cha kunywa pombe kwani unywaji wa pombe kupita kwaida, huathiri pia seli za kichwa na kuathiri uwezo wako wako wa kukumbuka mambo na kuwa makini. Unaweza kutumia red wine unapohitaji  kilevi kidogo.

6. Cheza game za kutumia akili kama “draft”, puzzle,   na mengineyo.

7. Lala masaa ya kutosha. Binadamu anatakiwa kulala masaa 7 mpaka 9 kila siku. Kulala usingizi wa kutosha huufanya ubongo wako kupata muda wa kutosha wa kupumzika na kuongeza uwezo wako wa kukumbuka mambo.

8. Epuka kuwa na msongo wa mawazo kwani huharibu baadhi ya seli za ubongo na kuathiri uwezo wa kumbukumbu zako.

9.Kula chakula chenye madini ya chuma kwa wingi hasa matunda na mbogamboga!


10. Kujipa muda wa  kukaa peke yako na kutafakari (Meditation). Kaa peke yako eneo lenye uoto wa asili kama bustanini, mtoni, au ufukweni na kujipa muda wa kutafakari. Hili ni moja ya mazoezi bora zaidi kwa ajili ya afya ya akili yako.

3 comments:

  1. Hii ndiyo mimi ninayoiita, life education (= after school education= informal education]. Na tuko weengi tu tunawotoa hii elimu, karibu buure. Nami naitoa hiyo elimu, kwa jina la Life Education Messages for All (LEMA] lakini maoni yangu mpaka sasa ni kwamba we have a reading culture problem in Tanzania and other developing countries. Tatizo ni kwamba kwenye maneno tunakubaliana kwamba elimu haina mwisho, lakini kwenye vitendo tunatofautiana. Sio wengi wa kutosha tunaochukua hatua za dhati kujiendeleza katika life education. Fikra potofu zilizoko mitaani ni kwamaba tuliachana na kusoma tulipomaliza shule au chuo. Wachache wanaojitahidi wanaishia kwenye daily newspaper..
    Prof. Pendaeli,

    ReplyDelete

Toa maoni yako

Copyright © 2014 Kumi Muhimu