KWA WANAUME:: VIJUE VITU 10 AMBAVYO WANAWAKE WANATAMANI SANA WANAUME WAVIJUE KUHUSU WAO!

KWA WANAUME:: VIJUE VITU 10 AMBAVYO WANAWAKE WANATAMANI SANA WANAUME WAVIJUE KUHUSU WAO!

Baada ya Kuwafanyia utafiti wanawake 100 wa kati ya miaka 18-40 maeneo mbalimbali Tanzania mbalimbali kujua ni vitu gani hasa wanavyotaka wagnaume wavijue, haya ndio tuliyoambiwa..

1.Ndugu wanaume , Tungependa muelewe kwamba, Tunahitaji zaidi muda na nyie kuliko hizo hela zenu.  Msifikiri furaha ya mwanamke ni pesa tu! Kumbe hata muda wako ni jambo la msingi sana kwetu.

2.Tunahitaji tuwe wa Muhimu zaidi kwenu kuliko hizo kazi zenu, marafiki zenu na hivyo vikao visivyoisha.

3.Tukifanya Kitu kwa ajili yenu, Tunapenda sana tujue kama kimekufurahisha. Neno moja la shukrani kwetu linamaana kubwa sana kwetu.

4. Kuwa na uwezo wa kufanya baadhi ya vitu kama kusafisha nyumba, kupika, nk  haimaanishi ni majukumu yetu na hampaswi kutusaidia. Hata sisi tunaweza kubadili tairi ya gari au kubadili taa iliyoungua!

5. Mavazi yetu sio bei raisi tu kama mnavyofikiri, Tungependa siku moja muongozane na sisi tunapoenda shopping muone gharama zetu

6. Tunapenda mtuambie mnatupenda mara nyingi muwezavyo sio mpka tuwaulize “Hivi unanipenda?”

7.Msizungumzie chochote Kuhusu Unene wetu au kutokuvutia! Tungependa tuambiwe tumependeza kila mara!

8.Tunamahitaji mengi zaidi ya vile mnavyofikiri

9. Tunapenda sana Muwe wasafi


10. Muwe wa kwanza kukumbuka siku yetu ya kuzaliwa, ina maana kubwa sana kwetu. 

Soma pia

kwa-wanaume-tu:: Makosa-haya-10-ya-uvaaji.yatakushushia CV yako

Wanawake::usitumie-maneno-haya-10.Unapoongea na Mpenzi wako (mwanaume)

3 comments:

  1. Hii ni kweli kabisa.Na wanawake wanapenda kubembelezwa na kudekezwa kama watoto.

    ReplyDelete
    Replies
    1. sawa sawa mdau! ni maneno yaliyotoka kwa wanawake wenyewe!

      Delete
  2. Napenda wanawake wenyewe wakideka aisee... wenyew wanapenda kubembelezwa

    ReplyDelete

Toa maoni yako

Copyright © 2014 Kumi Muhimu