WANAWAKE:::: USITUMIE MANENO HAYA 10 UNAPOONGEA NA MWANAUME (MPENZI WAKO)

WANAWAKE:::: USITUMIE MANENO HAYA 10 UNAPOONGEA NA MWANAUME (MPENZI WAKO)

1.Nimepitia wanaume wengi ila wewe ni zaidi ya wote!
Wanaume hawapendi kujua umeshakuwa na uhusiano na wanaume wangapi hapo kabla kwani hujisikia vibaya kujua mpenzi wake alishawahi kuwa na mtu Fulani!

2. Huwezi wewe!
Hakuna kitu mwanaume hapendi  kusikia kama kuonekana ameshindwa au hawezi kufanya jambo Fulani! Hutakiwi kumueleza moja kwa moja kwamba hana uwezo wa kufanya jambo Fulani.

3.Yule kaka ni mtu makini sana  Tengeneza  urafiki nae
Ukitaka kugombana na mwanaume, basi mlinganishe na mwanaume mwingine. Usionyeshe kamwe kwamba kuna mwanaume ambaye ungependa awe kama yeye!


4.Nampenda rafiki yako! Ni mchangamfu sana
Japo hutakuwa na maana yeyote mbaya, lakini maneno hayo huwa ni magumu kwa mwanaume kuyasikia. Ongea maneno hayo pale tu anapoanza yeye kuzungumzia mazuri ya mtu huyo!

5. Nikulipie? (mbele za watu)
Daima mwanaume hupenda aonekane juu ya mwanamke mbele ya watu hata kama ni mnyonge mkiwa peke yenu. Kama unalipa kwa niaba yake, basi fanya kimya kimya au mtumie hata ujumbe mfupi kumuarifu juu ya hilo.

6. Mimi na hiyo timu yako nani bora? (unapomkataza asiende mpirani)
Kama unavyopenda kuhangaikia nywele zako, kucha nk mwanaume nae ana vitu avipendavyo. Daima usimuonyeshe kwamba hicho anachokipenda hakina umuhimu wowote

7. Huwezi Kunifanya lolote  (Mbele za watu)
Hata kama ni mnyonge wako mkiwa peke yenu, Mwanaume anaweza kukugeuka na hata kukuumiza endapo tu utaionyesha jamii kwamba yeye ni mnyonge wako!

8. Mpenzi wangu wa zaman alikuwa ananifanyia hivi…
Hakuna mwanaume anaependa kusikia lolote kuhusu mpenzi wa zaman wa mke/msichana wake. Hasa kuzungumzia mazuri kadhaa au kumfananisha na yeye kwa namna yoyote ile.

9.Hunipendi  kama mtu Fulani anavyompenda mpenzi wake! Au wale wanapendana zaidi kuliko hata sisi!

10. Tumia akili/ usiwe mnafiki/ acha uvivu. 
Maneno haya yanaweza kuleta ugonvi usioisha hata kama ameshawahi kukuambia maneno hayo pia!


1 comment:

Toa maoni yako

Copyright © 2014 Kumi Muhimu