WANAWAKE:SABABU KUMI KWAMBA MPENZI WAKO NI “MWANAUME” SIO “MVULANA”
1.Anapoishi,
Pana Muonekano wa “Nyumbani” sio “Nyumba” yaani sio lazima awe na mali nyingi,
wala si lazima iwe nyumba yake. Jambo la msingi ni je, anajali makazi yake?
Hata kama anaishi chumba kimoja, je, sakafu ya nyumba ina rangi yake ya asili?
2.Ana
Malengo ya Maisha na Kufanya anachokipenda bila kujali anakutana na changamoto
gani. Mwanaume mwenye ukomavu kiakili siku zote anamipango ya kutoka hatua A
kwenda B na kuna kitu cha ndani kinachomvuta afanye hivyo.
3.Anauwezo
wa kujitegemea kimaisha, na yeye mwenyewe kiujumla. Yaani hata kama amelewa hategemei mtu ampeleke
nyumbani.
4.Ana
Msimamo na mipaka yake, Si kila utakachomuambia anakubaliana nacho.
5.Siku
zote anajua anataka nini, vipaumbele vyake maishani, na wewe ni mmoja wa
vipaumbele hivyo. La sivyo unaishi na Mvulana si MwanaUme
6.Hakuambii
Huwezi siku zote, Mwanaume wa kweli anakupa moyo, na anamuda wa Kukusaidia kutimiza
ndoto zako, anajua mahitaji ya mpenzi wake na kuyatengea Muda Fulani.
7.Hufanya
Maamuzi, japo haoni tatizo kukuacha ufanye baadhi ya maamuzi pia.
8.Anajua
Thamani yako, Hakuambii tu anakupenda, bali hukuonyesha ni jinsi gani
anakupenda.
9.Hakuonei
aibu.
10.
Anajipenda, anajituma, Anavaa na kufanya mambo kiutu uzima na ana malengo yake
ya baadae.
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako