LICHA YA MAISHA MAGUMU, KWANINI WATANZANIA WENGI WALIO NJE HAWATAKI KURUDI NYUMBANI?. SOMA SABABU HIZI 10

LICHA YA MAISHA MAGUMU, KWANINI WATANZANIA WENGI WALIO NJE HAWATAKI KURUDI NYUMBANI?. SOMA SABABU HIZI 10

Safari ya kutoka Afrika kwenda bara linguine imekuwa ikichukuliwa kama bahati, na mtu anayekwenda Ulaya, marekani au hata afrika ya kusini amekuwa akionekana kama amepiga hatua kubwa na pengine amashapiga teke umasikini. Hebu tuliangalie kwa jicho la Pili, Je wajua walioko Nje ya nchi wanafanya Kazi zipi? Sitaki kwenda sana Huko (Maana nagusa “ajira” za watu), lakini ukweli ni kwamba, Wengi wa ndugu  na jamaa zetu walioko nje wana Maisha Magumu, lakini pia kuna kundi kubwa la watu wenye uwezo wa kielimu na kipato cha kuweza  kuisaidia nchi yao lakini suala la kurudi nyumbani ni “ndoto” kwao. Wengi wanakwamishwa ni vitu vifuatavyo 10.



1.Ntawezaje kurudi “bongo” wakati sijafanikiwa?
Hii hasa  ni kwa wale wasiokuwa na ajira rasmi huko walipo. Pengine wanaelimu ya kutosha ila wakishafikiria ndugu zao nyumbani, matarajio waliyonayo juu ya kijana wao aliye nje, wanakata tamaa ya kurudi na kusubiri pengine hali itakapokuwa nzuri angalau kupata kidogo atakachoweza kununua zawadi kadhaa kwa ajili ya lile kundi litakalompoke airport!.


2.Ntakwepa vipi tatizo la kuombwa hela na Kuchukuliwa kama Mtu wa Kawaida?
Uwe una kipato au huna kipato, Suala ni umetoka nje ya nchi lazima utakuwa na hela, una akili sana na ukisema huna hela, basi utaulizwa ulienda kufanya nini ulaya? Hivyo ukirudi toka nje ya nchi tegemea kukabidhiwa majukumu makubwa na hili ndilo linafanya watu kutotaka kurudi nyumbani.

3.Ntapata vipi kazi Tanzania?
Wajua Tatizo linakuwa wapi?  Mtu anaishi Marekani, amesoma,  anataka kurudi nyumbani apate kazi, akiangalia kwenye mtandao  anakuta kazi zinatangazwa, anaziweza vizuri, lakini zinahitaji uzoefu miaka mitatu, Ndio anao uzoefu kazini, lakini kazi aliyokuwa anafanya ni kutengeneza bustani! No hawataweza kuniajiri, Ngoja nibaki hukuhuku labda maisha yataendelea vizuri!.



4.Sitaki Kuishi kwa wazazi wangu, Nina Familia, Ntawezaje Kupata Nyumba nyingine?
Kuna Idadi kubwa ya watu wanaoishi na familia zao nchini Marekani, wana watoto kule, na wameshazoea kuishi hivyo. Maisha yanapokuwa magumu, inakuwa ngumu kwa wao kurudi tena nyumbani. Suala la kusafirisha familia ni gumu, pia mahali pa kukaa ni tatizo linguine kwani kwa sasa huwezi tena kuishi na wazazi wako.


5.Ntaweza Kufanya Kazi ninazozifanya nikirudi nyumbani? Au Kuna Kazi zinazohusiana na hiki nilichosomea?
Mazingira ya kazi katika nchi za Magharibi ni tofauti kabisa na afrika. mathalani, Mtu amesomea uokozi (lifeguard) na kuna kazi zinapatikana Huko, Tatizo linakuja kwamba, Kiafrika, suala la kujiokoa na usalama wako uko mikononi mwako kwa asilimia 99 (99%) hivyo kumuajiri mtu aliyesomea kuokoa watu kwetu ni matumizi mabaya ya fedha. Hili pia ndio sababu inayomfanya mtu aone ni bora abaki ugenini japo maisha ni Magumu.

6.Ntapata Shule nzuri kwa ajili ya wanangu? Na je watazoea kuishi Tanzania?
Hii huwa sehemu ngumu zaidi kwa wenzetu hasa ikishafika kipindi kwamba maisha ni magumu, hawawezi kuendelea kukaa ugenini lakini je, watoto watasoma shule gani? Na wameshazoea maisha ya kimagharibi, sasa je watafurahia kuishi ugenini?.



7.Ninampenzi wa huku, atakubali nirudi nae nyumbani?
Hapa ndipo penye shida, Hata kama  atakubali, je  wazazi wake watamkubali mpenzi wake huyo asiyejua mila na tamaduni za nyumbani? Hivyo ili kumfurahisha mpenzi wake, huona bora aendelee kukaa ugenini hata kama maisha yake ni magumu.





8.Nimeshakuwa “Mzungu” Siwezi tena  “uswahili”. Ntapata wapi bima za afya nk?
Kuna aina mbili za Ubaguzi, ubaguzi wa kuzaliwa nao, na ubaguzi wa kuurithi/kujifunza,  Huu ubaguzi wa kurithi ndio unawapata sana ndugu zetu walio nchi za magharibi, na wana kipato kizuri. Kwanza wanasafiri kwenda nje, baadae wanasahau yote ya nyumbani na licha ya “uweusi” wao wanaanza kujiona wao ni wazungu na hawawezi tena kuishi maisha bila baadhi ya vitu na kusahau kabisa nyumbani.

9.Nyumbani Kila Kitu Ni siasa na Kujuana!
Kuna Watanzania Wengi sana wanaotamani warudi nyumbani kuanzisha biashara au miradi mbalimbali lakini wanakumbuka kuwa ili kufanya chochote nyumbani lazima ujuane na watu Fulani, au “uwaone” watu Fulani la sivyo hakuna utakachoweza kufanya.

10. Wengi waliorudi Maisha yaliwashinda na wakachekwa! (wakarudi "abroad" kubeba mabox)
Kuna wengine hawataki kurudi nyumbani kwa kuwa tu wameona mifano ya baadhi ya watu waliorudi Tanzania na maisha yakawa magumu kwao na wao wakaingiwa na uoga!.



0 comments:

Post a Comment

Toa maoni yako

Copyright © 2014 Kumi Muhimu