MAAJABU KUMI YA SOKA USIYOYAJUA
1.Mwanasoka mkongwe wa brazil pele, alijipatia jina
hilo la utani lenye maana katika lugha ya kibrazil na kireno “ miguu sita” (six
feet),kutokana na kuwa na vidole sita katika kila mguu.
2.Mwana soka anakimbia kilomita zipatazo kumi (10)
katika mchezo mmoja.
3.Mwanasoka wa kibrazil, Ronaldinho ndio mfungaji
anayekumbukwa zaidi kwa kufunga mabao mengi duniani, alifunga mabao 23 akiwa na
umri wa miaka 13 tu.
4.Mnamo mwaka 1998 Radi iliua wachezaji wote kumi na
moja (11) wa timu moja na kuacha wachezaji wa timu pinzani wakati wa mchezo
nchini DRC na kudhuru watazamaji wapatao thelathini.
5.Mnamo mwaka 1964 simu aliyopokea mwamuzi wa mchezo
(refa) akiwa uwanjani huko nchini Peru ilisababisha vurugu iliyopelekea watu
mia tatu (300) kufariki.
6.Washabiki wa soka nchini Columbia waingia na
jeneza uwanjani la mshabiki mwenzao aliyeuawa kwa kupigwa risasi siku ya
kuwania kuingia fainali akiwa na umri wa miaka17. Washabiki hao waliingia nae
siku ya fainali.
7.Mnamo mwaka 1966 kombe la dunia liliibiwa na
baadae mbwa akalipata siku chache kabla
ya mshindano hayo kuanza. Kombe la dunia kwa mara ya kwanza lilitengenezwa kwa
makaratasi na kubadilishwa baada ya kuharibiwa na mvua kali iliyonyesha. Siku
hizi kombe hilo linatengenezwa na zahabu yenye uzito upatao kilo 4.97.
8.Katika kombe la dunia mwaka 1950, timu ya Soka ya India ilitaka
kucheza peku, shirikisho la soka ulimwenguni (FIFA) likagoma. Timu hiyo
ikasusia mashindano hayo!
9.Pele alipokwenda Nigeria kucheza soka katika
mchezo wa hisani mnamo mwaka 1967, pande mbili zinapigana vita, zilikubaliana
kusimamisha vita kwa muda wa masaa 48.
10.Mrtinho Eduardo Orige kutoka Brazil ndio mchezaji
pekee kuchezea mpira kwa muda mrefu zaidi duniani! Alichezea mpira kwa muda wa
masaa 19.5, alivunja record hiyo mnamo mwaka 2003.
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako