UNAZIKUMBUKA SHERIA HIZI 10 ZA MPIRA WA MIGUU WAKATI TUKIWA WATOTO? cheka hapa!

UNAZIKUMBUKA SHERIA HIZI 10 ZA MPIRA WA MIGUU WAKATI TUKIWA WATOTO? cheka hapa!


1. Kona
Si lazima Kutumia mguu unapopiga kona, Ukiona mazingira hayakuruhusu, rusha kwa mikono (unaweza kutumia Mkono mmoja kama mpira ni mdogo)

2.Mwenye Mpira
 Mwenye mpira ndiye ana maamuzi ya nani acheze na
nani asicheze, ni marufuku kumtoa Mwenye mpira hata akicheza vibaya. Anaruhusiwa kukutoa endapo hutampa pasi (hatakama ulifunga)


3.Upangaji wa Kikosi
Mwenye mwili mkubwa huyo ni beki mnene lazima awe golikipa,Ila mwenye mpira anaruhusiwa kupanga upya, na yeye lazima awe mshambuliaji


4.Penati
Itatokea tu pale mchezaji akiumia sana, akalia na kutoka damu. (mara nyingi hatoendelea na mpira)

5.Kuotea (offside)
Hakuna Kuotea, Free kick itapigwa pale tu mtu akishika mpira.


6. Refa
Ni Yule mchezaji mbabe, au mwenye mpira, ila mchezaji anaweza kuzunguka

na mpira hata nyuma ya goli.

Kubadili Mchezaji
7. Inaruhusiwa kubadili Mchezaji endapo ataitwa kwao na akirudi, ataendelea na nafasi yake. Pia ni ruksa kubadili golikipa kama penati ikitokea na baada ya penati golikipa anaweza kuendelea yule wa mwanzo.

8.Wachezaji wa akiba
Wale ambao wamekosa namba kazi yao ni kufata mpira ukitoka, au kutungua mpura endapo utanasa kwenye mti huku wakisubiria mchezaji aitwe kwao na wao wapate nafasi.


9.Jezi
Upande wa mwenye mpira watavaa mashati na wengine watavua. Suala la viatu, Mwenye Mpira anaamua Wote Mcheze peku au na viatu, akikasirika, mechi ndo itakua imefika mwisho

10.Mpira Kumalizika
Mechi itaisha pale tu Mwenye mpira ataitwa nyumbani,atakapochoka, au kama kila mchezaji atakua amechoka, au giza kuingia.

0 comments:

Post a Comment

Toa maoni yako

Copyright © 2014 Kumi Muhimu