1.Jifunze kukumbuka majina ya watu. Sio kila mtu anapendw
aitwe “wee kaka/dada”, “ankoo”, “mzee”. Kukumbuka
majina ya watu situ itakupa heshima, bali pia utaonekana ni mtu makini na unayejali.
2.Kumsifia mtu anapofanya kitu kizuri (compliments). Nani
hapendi kusifiwa?
3. Jifunze namna ya kufikisha habari mbaya/ ya kusikitisha
kama msiba, ajali nk
4. Usipende kuangalia saa unapoongea na mtu. Hasa anapokuelezea
tatizo lake. Badala yake kama unaona anakuchelewesha, tengeneza mazingira ya
kupigiwa simu ili uondoke.
5. Jifunze Kutabasamu unapopigwa picha! Ina maana kubwa sana
J
6. Jifunze kuepuka ugonvi. Na ukiingia kwenye Ugonvi kwa
bahati mbaya basi jifunze kushuka la sivyo hakikisha unashinda ugonvi huo.
7. Jifunze kuwa msikilizaji mzuri. Kumbuka, Kila mtu
anapenda kusikilizwa.
8. jifunze kusema samahani na ahsante. Epuka kutumia maneno
kama “najua” au “mimi pia” badala yake elezea unajua kiasi gani badala ya
kutumia maneno hayo moja kwa moja!
9. Jifunze kuonyesha unakumbuka matatizo ya watu waliyokueleza hapo
kabla na usisahau kuwauliza wamefikia wapi mnapokutana. Mfano kama alisema ana
mgonjwa basi kumbuka kumuuliza hali ya mgonjwa. Kumbuka binadamu tunapenda
kuonewa huruma.
10. Jifunze namna ya kumuonyesha ukarimu mgeni. Pia jifunze
kuwa mgeni bora pale unapokaribishwa na mwenyeji wako
Soma pia
hilo la kutabasanu kazi kwelikweli
ReplyDeletemkuu, namba tano duuh!
ReplyDeleteNahisi nina matatizo, Ksb najisikia vibaya sana mtu mwingine anaponiita "wee fulan, kaka/dada" ...nachukia kuanza na neno "wee"
ReplyDeletenapenda uanze na samahan.......
Huna Matatizo ndugu! hakuna anayependa hivo!
DeleteKuna alimwambia mfanyakaz mwenzie kuwa ," bado upo Latino si umefiwa na baba yako msibani" . maskin kumbe mfiwa alikuwa hana taarifa, ilisikitisha sana kilichoendelea baada ya hiyo taarifa isiyo na chembe ya huruma.
ReplyDeleteDaah hiyo noma sana!
Delete