TANGAZO WANAMUZIKI 10 MATAJIRI ZAIDI AFRIKA MWAKA 2014
Saturday 4, Jan 2025

WANAMUZIKI 10 MATAJIRI ZAIDI AFRIKA MWAKA 2014

kamil
10.Jose Chameleon

Ni mwanamuziki wa Uganda Mwenye mafanikio zaidi, anamiliki jumba la kisasa, magari manne (yakiwemo Escalade, Benz na Cadillac). Ndiye mwanamuziki tajiri zaidi afrika mashariki kwa sasa.









davido8
9.Davido
Ndiye mwanamuziki mwenye umaarufu zaidi kwa sasa akitokea nchini Nigeria. Ameshinda tuzo ya mwanamuziki bora kutoka Africa kwenye tuzo za  BET. Mpaka sasa ana tuzo 17 akiwa na miaka mitatu tu kwenye muziki. Utajiri wake unatokana sana na baba yake ambaye ni bilionea maarufu nchini Nigeria.



220px-Hugh_Masekela_2009
8.Hugh Masekela
Anatokea Africa ya Kusini, ni mpiga  vyombo  vya aina zote! Pia ni chaguo namba moja la Raisi wa S.A bwana Jacob Zuma







2face
7. 2face
Ni maarufu zaidi kwa wimbo wake wa “African queen”. Alijitoa kwenye kundi lake  mwaka 2004 na hapo ndipo mafanikio yake yalianza kuongezeka kwa kasi kubwaa. Anamiliki ardhi kubwa sana na huchaji dola 80,000 kwa kila show (kama shilingi 140,000,000) za kitanzania






download
6.Salif Keita.
Anajulikana kama  “Sauti ya dhahabu ya Africa”. Ni mwanamuziki  albino anaetokea nchini Mali. Ni mwanamuziki mwenye mali nyingi zaidi ulaya, pia anamiliki kisiwa kidogo!









fally
5.Fally Ipupa
Ni mwanamuziki wa DRC anayeishi nchini ufaransa. Alikuwa kundi moja na Mfalme Koffi olomide na baadae kuanza kufanya kazi mwenyewe mwaka 2006. Ameshinda Tuzo za Kora na MTV, ndiye mwanamuziki wa kiafrika anayefanya shoo kubwa zaidi jijini Paris.







koffi
4.Koffi Olomide
Analipwa kuanzia euro laki moja kwa shoo moja (Zaidi ya milioni 200). Album yake moja imeingia katika album bora zaidi 1000 za wakati wote.





download+(1)
3.D’Banj
a.k.a  koko master! Ni mwanamuziki pekee wa kiafrica Kusainiwa kwenye label ya “GOOD” inayomilikiwa na Kanye West! Nyimbo zake zinapigwa katika klabu zote duniani. Anamiliki klabu ya usiku, kiwanda cha maji cha “koko water”




ps
2.P.Square
Ndio Wanamuziki Maarufu Zaidi kwa Afrika. Wameuza album nyingi zaidi kuliko mwanamuziki mwingine afrika, shoo  ya p.square inagharimu dola 150,000 (milioni 250) kwa shoo moja. Wanamiliki mali zenye thamani ya Dola milioni tatu (sh bilioni 5 za kitanzania).




you
1.Youssou N'Dour
Ndiye mwanamuziki Tajiri zaidi Afrika! Tofauti na weni wanavyodhani! Anamiliki Kituo cha Redio na TV nchini Senegal,aliandika wimbo wa kombe la dunia mwaka 1998, na aliwahi kuwa waziri wan chi yake mwaka 2012

0 comments:

Post a Comment

Toa maoni yako

Copyright © 2014 Kumi Muhimu