MAJIBU KUMI YATAKAYOKUVUNJA MBAVU UKIMSHTUA MTU ALIYEPITIWA NA USINGIZI OFISINI/DARASANI

MAJIBU KUMI YATAKAYOKUVUNJA MBAVU UKIMSHTUA MTU ALIYEPITIWA NA USINGIZI OFISINI/DARASANI


DARASANI
1.Daaah! inabidi niache kusoma mpaka usiku maana jana nimesoma wee acha tu!

2. mmh hili somo litaniua bwana yaani natafakari  hapa wala sipati jibu! (kumbe alilala)

3. Bora umekuja hivi ndo nilikua nakusubiri wewe tufanye discussion daah!

4. Aisee ile dawa niliyokunywa jana usiku siitumii tena!



5. Aaaaah! Mbona umeni “interrupt?” yaani ndo nilikua nakaribia kupata lile jibu la swali tuliloachiwa!

OFISINI SASA
6. Yaani hata dokta aliniambia jana  kwamba hii ingetokea! (kana kwamba anaumwa au alipitia hospitali)

7. Yaani hapa nalipiza ya jana usiku maana usiku mzima  niliota niko ofisini nafanya kazi!

8.   ……Amen!   (kana kwamba alikuwa anasali)

9. Ni bosi anayeniita?? (kasahau kuwa bosi amesafiri)


10. Aisee kumbe keyboard ya kompyuta inalia hivi ukiweka sikio karibu!

Soma Pia
aina-ya-watu-na-vitu-10-vinavyoudhi.zaidi maofisini

2 comments:

Toa maoni yako

Copyright © 2014 Kumi Muhimu