WACHEZAJI KUMI WALIOKUBUHU KWA KUVUTA SIGARA

WACHEZAJI KUMI WALIOKUBUHU KWA KUVUTA SIGARA

Licha ya Sigara kuwa adui mkubwa wa afya na hata michezo pia, wachezaji wengi wa soka wamekua wakiendeshwa sana na “kilevi” hicho huku wengine ikiwa ni sehemu ya maisha yao! Hapa tumekuandalia list fupi ya baadhi ya wachezaji wanaotumia sigara kupindukia
.







1.Mario Balotelli
Wengi wanatarajia kumuona mtukutu huyu kwenye hii orodha, alishawahi kutishiwa na Roberto Mancini kwamba  angetimuliwa katika klabu ya man city kwa tabia yake ya kuvuta sana sigara. Pia inasemekana hii ni moja ya sababu ya Mario kuicha klabu yake hiyo ya zamani.





2. Mesut Ozil
Licha ya kuonekana mpole sana machoni, Ozil ni moja kati ya watumiaji mahiri wa sigara kitu ambacho hakimfurahishi kocha wake arsene wenger .







3.Wayne rooney
Aligusa vichwa vingi sana vya habari nchini Uingereza baada ya picha yake kusambaa akionekana anavuta sigara kwenye bwawa la kuogelea mwaka 2010. Toka hapo haijawa siri tena kwamba mshambuliaji huyu wa man united ni mtumiaji wa sigara



4.Ashley Cole
Kama kuna mtu anagonga vichwa vya habari kwa wingi kutokana na uvutaji wa sigara, basi Ashley cole anaongoza. Huanza kuvuta tu baada ya kupiga mpira wa mwisho kuashiria msimu umeisha. Sigara ndiye rafiki yake wa karibu hasa anapokuwa mapumzikoni




5. Zinedine Zidane
Licha ya kushiriki kwenye kampeni ya kuzuia uvutaji wa sigara mwaka 2002, Zidanne ameonekana mara kadhaa akipuliza moshi huo hatari kwa afya ya binadamu








6.Jack Wilshire
Alikumbwa na vikwazo vikubwa baada ya kuonekana akivuta sigara nje ya klabu moja ya usiku na kumuudhi sana  meneja wake Arsene Wenger . Japo huyohuyo wenger aliibuka na kumsajili mvutaji mwingine Mesut ozil



7. Dimitar Berbatov
Japokuwa yeye hupinga na kudai huweka sigara mdomoni kwa ajili ya utanashat tu, marafiki na wachezaji wenzake mara kadhaa wamekiri kuwa berbatov huvuta sigara kila anapokuwa hayumo kikosini.



8. Maradona
Licha ya sigara, Mkongwe huyu pia amejiingiza katika matumizi ya tumbaku na ulevi mwingine kadhaa

9. Fabien Barthez

 10. Johan Cruyff
Mkongwe huyu wa Uholanzi pengine ndiye anaeshikilia rekodi ya mwanasoka aliyevuta zaidi sigara (ukiacha wachezaji wa kibongo) aliyekuwa akivuta sigara 20 kwa siku akiwa mapumzikoni. Kwa sasa ameacha baada ya kuugua sana


NB: Lionel Messi havuti Sigara (picha hapo juu alikuwa akila pipi)   :) :)

soma pia


0 comments:

Post a Comment

Toa maoni yako

Copyright © 2014 Kumi Muhimu