EPUKA LUGHA HIZI ZA MWILI (BODY LANGUAGES) WAKATI WA KUFANYA USAILI (INTERVIEW)
1.Epuka Kukunja mikono yako Kifuani hii huonyesha kujiamini kupita kiasi, dharau au wakati mwingine huashiria kutokubaliana na kile kinachozungumzwa
2. Kama umesimama, jitahidi unyooke, epuka kuegamia
ukuta au kupishanisha miguu (kuchora alama ya X). Kama umekaa usiegamie sana
kiti kwani hii huonyesha ishara ya uvivu. Kaa ukiwa umenyooka
3. Epuka kuwa wakwanza kukwepesha macho kwa haraka
unapomuangalia anayekufanyia usaili au aliyekuuliza swali. Hii huonyesha kukosa
kujiamin au tabia ya udokozi. Daima angalia mbele usiiname chini unapoulizwa
maswali
4. USITAFUNE KITU chochote mdomoni iwe pipi au vidole vyako (hasa kwa wanawake)
4. USITAFUNE KITU chochote mdomoni iwe pipi au vidole vyako (hasa kwa wanawake)
5.Usionyeshe Ishara yoyote mbaya unapomzungumzia muajiri wako aliyepita (hata kama ndiye sababu ya wewe kuacha kazi)
6.Usiwanyooshe vidole wanaokufanyia usail
7. Usitikise sana kichwa kupita kiasi. Ni vizuri kutikisa kichwa unapoonyesha kuelewa kile unachoambiwa, lakini mara nyingine inawezekana ukaulizwa swali la mtego ambalo hutakiwi kukubali!
8. Usiweke mikono nyuma au mfukoni unapoingia ndani au ukiwa umesimama. Hii hunyesha hali ya kutotaka kuwa muwazi, au majivuno.
9.Unachokizungumza kifanane na uso wako. Mfano unapozungumzia
kitu kinachokufurahisha halafu una sura nzito, una hatari! Jitahidi kutoa tabasamu
kila unapoulizwa swali au kuelezea kitu
10.Usiangalie sana juu ishara ya kukumbuka kitu. Hii huonyesha kutokuwa na hakika ya kile unachokizungumza!
Soma Pia
Hakikisha-unaweza-kujibu-maswali-haya kabla ya interview