WAJUA NINI HUTOKEA BAADA YA KUACHA KUVUTA SIGARA? TAZAMA HATUA HIZI KUMI
Unafikiria kuacha sigara? ….Yees! wazo zuri. Kwanini? Kwa sababu
utaanza kuona faida za kuacha kuvuta sigara ndani ya dakika ishirini tu baada
ya kuacha! Wajua inachukua muda gani mpaka kiasi cha nicotine kutoka mwilini
mwako? Soma haya…
1.Dakika ishirini (20) tu, baada ya kuacha kuvuta sigara
mapigo yako ya moyo huanza kurudi katika hali ya kawaida
2. Masaa mawili baada ya kuacha kuvuta sigara, mzunguko wako
wa damu hurudi katika hali ya kawaida. Kiwango cha nicotine hushuka mpaka
asilimia 6.2
3. Wajua wavuta sigara wana hasira za haraka? Baada tu ya
masaa 24 yaani siku moja baada ya kuacha sigara, mvutaji hujisikia mwenye amani
na akikaa hivyo kwa wiki moja zaidi hujisikia katika hali bora zaidi.
4. baada ya siku mbili tu toka uache kuvuta sigara, neva
zilizoanza kufa huanza kurudi katika hali yake na kiwango cha kunusa na uwezo
wa ulimi kutambua ladha huongezeka!
5. Siku tatu baadae mwili wako hautajisikia kuwa na nicotine
tena kwa asilimia 100% japo bado itakuwepo kwa kiasi Fulani. Na utaanza
kupunguza uwezekano wa kupata magonjwa kama TB au mshtuko wa moyo.
6. Wiki moja tu baada ya kuacha sigara utakuwa na uwezo wa
kufanya shughuli yoyote ya kutumia nguvu ambayo mwanzo ulikuwa ukichoka kwa
haraka baada tu ya kufanya hivyo.
7. Mwezi mmoja mpaka mitatu baada ya kuacha, mapafu yako
huanza kuwa safi na kurudi katika hali yake ya kawaida
8. Mwaka mmoja baada ya kuacha sigara, hatari yako kupata
magonjwa kama TB na mshtuko wa moja hushuka mpaka asilimia 50% kulinganisha na
mvutaji!
9. Miaka mitano baada
ya kuacha sigara Utakuwa umepunguza kwa kiasi kikubwa uwezekano wa kupata
kiharusi. Na kupunguza kama si kuondoa kabisa
uwezekano wa kupata TB (inategemeana umevuta kwa mda gani)
10. Miaka Kumi na zaidi baada ya kuacha sigara, tapunguza
uwezekano wa kupata kansa ya mapafu, na madhara hayataonekana mwilini mwako kwa
asilimia karibu mia moja (100%) na Utakuwa na furaha zaidi maishani.