WAJUE WATU KUMI (10) MASHUHURI WALIOZALIWA TANZANIA LAKINI SIO WATANZANIA

WAJUE WATU KUMI (10) MASHUHURI WALIOZALIWA TANZANIA LAKINI SIO WATANZANIA

Licha ya Kuwa na watu kadhaa mashuhuri duniani, Nchi Ya Tanzania imezalisha watu kadhaa mashuhuri ambao sio watanzania lakini wamezaliwa Tanzania.
 Wafuatao ni watu Kumi Waliozaliwa Tanzania na watanzania Hawawafahamu.

1. Marin Hinkle: Kama wewe ni Mfuatiliaji Mzuri wa Sinema za Hollywood, bila shaka utakuwa unamfahamu Marin Hinkle aliyeigiza sinema kadhaa zikiwemo Once and Again (1999),  Two and a Half Men (2003) na  Law & Order: Special Victims Unit (1999)  :  Marin Hinkle aliwahi pia kutajwa mmoja kati ya "The Queen's Of TV Historyakishika nafasi ya kwanza mbele ya watu kama Tyra Banks. Alizaliwa Tanzania wazazi wake wakiwa askari wa kulinda amani na baadae kuhamia Boston





2  Rachel Luttrell: Kama ilivyo Kwa Marin Hinkle, Rachel pia ni muigizaji maarufu wa hollywood aliyezaliwa Jijini Dar es Salaam akiwa mtoto wa Daktari Maarufu wa Kabila la Wasambaa Shenkunde Luttrell. Akiwa na Umri wa miaka mitano, Familia ya Rachel ilihamia Toronto Canada. Alikojifunza kupiga piano na kipaji chake cha uigizaji kuonekana.



3. Freddie Mercury: (1946–1991) Ni Muimbaji maarufu wa Uingerezao aliyefariki mwaka 1991 kwa ugonjwa wa UKIMWI. alifahamika sana kwa staili yake ya kuweka microphone chini ya mkanda wake.alizaliwa zanzibar na kusoma india, baadae familia yake ilihamia uingereza.


4.Adam Nditi: mwanasoka aliyezaliwa Zanzibar anayecheza soka la kulipwa Katika klabu ya watoto chelsea ana uraia wa uingereza.






5.Alan Johnston: Muandishi wa Habari Mashuhuri Duniani akifanya Kazi BBC. alipata umaarufu zaidi alipotekwa na wanajeshi wa hamas mwaka 2007


6.Dimitri Panayotopoulos- Mfanyabiashara na Tajiri aliyezaliwa nchini Tanzania

7.Harold O'Neal- Mtayarishaji wa muziki wa Kimarekani, 

8.Ian Iqbal Rashid- Muandishi na Mshairi

9.David Adjaye: Muhandisi Mashuhuri Duniani. alizaliwa Tanzania, ana uraia wa Uingereza.

10.Luke Adams
Mshindi mara tatu wa mashindano ya olympic aliyezaliwa Mvumi Dodoma. Ni Raia wa Australia 

soma pia


je-wajua-watanzania-hutafuta-nini.kwenye mtandao?



Copyright © 2014 Kumi Muhimu