EPUKA MAKOSA HAYA UNAPOANDIKA CV YAKO (Curriculum vitae)
2.Usiongeze vitu usivyoweza kuvifanya kwani vitakuumbua siku
ya kufanya usaili na kuonekana hujui mengine yote!
3. Epuka kuonekana umefanya kazi nyingi kwa kipindi kifupi
kifupi. Mathalani umemaliza chuo mwaka 2012, umeshafanya kazi na makampuni
manne tofauti mpaka kufikia mwaka 2014
4. Wasifu wako hautakiwi kuwa na vifupisho bila kuchanganua mfano, nimefanya kazi TRA, AMD, na NIC. Sio
wote wanayajua makampuni hayo.
5. Usisahau kuweka mawasiliano yako hasa namba ya simu na
anuani yako ya barua pepe
6. Kuweka namba za wadhamini ambazo hazipatikani, pengine walishabadili
namba hizo ila kutokana na kwamba huna mawasiliano nao, hujui chochote!
7.Mpangilio mbovu wa wasifu wako, na kushindwa kuelezea
kiundani uwezo wako.
8. Epuka kuandika wasifu usioendana na matakwa ya kule
unakoupeleka unapoomba kazi. Daima fanya marekebisho kila unapoomba kazi sehemu
nyingine.
9. Epuka kuiga wasifu wa mtu mwingine au kukopi kutoka kwenye mitandao matokeo yake
mwajiri anakutana na CV kadhaa zinazofanana!
10. Daima panga karatasi zako vizuri kufuata mtiririko
kuepuka kumchnganya msomaji na matokeo yake ni kuitupa kapuni na kuendelea na
wengine.