MUHIMU: MAKOSA 10 AMBAYO WAZAZI WA KITANZANIA HUYAFANYA KWENYE MALEZI
Una habari kwamba brooklyn
beckham (15), mtoto wa bilionea na mwanasoka wa zamani maarufu duniani David
Beckam anafanya kazi mgahawani? Tena analipwa euro 2.6 kwa saa Yaani Sh 6000/=
za kitanzania.
Je baba yake asingeweza kumpa mshahara mara 10 ya huo tena kwa kukaa tu ndani?. Utakubaliana na mimi kwamba wazazi wa sasa wanawekeza zaidi katika maisha ya watoto wao kuliko kizazi chochote kile kilichowahi kutokea! Pengine ni mabadiliko ya kimaisha, lakini Je, hiki tunachokiita “malezi ya kisasa” Kinaweza kuleta Madhara gani Baadae? Je, tunatengeneza taifa la namna gani baadae? Nia yangu sio kumnyooshea mtu kidole bali kujaribu kujenga uelewa zaidi katika jamii yafuatayo ni baadhi ya mambo kumi wazazi hukosea katika malezi:

1.Tunalea “Mtoto
tunayemtaka” sio “mtoto tuliyenae”
Wazazi wengi hulea
watoto wao wakitaka kuwachagulia aina Fulani ya maisha bila kujali mtoto
walienae anaweza vitu ganina na kupenda
nini. Badala yake kila mzazi huamini mwanae atakua na tabia kama za kwake na
pengine atakua na akili na uwezo zaidi au hulazimisha mwanae awe na kipaji
Fulani eti tu kawa kuwa mzazi ana kipaji/kalama hiyo! Kumbe ingekuwa hivyo basi
tusingehangaika kutafuta viongozi, wanasoka au wasanii bora kwani tungewatumia
watoto wao tu!
2. Kusahau Kuwa Vitendo vyetu (wazazi) vinaongea kwa sauti
kubwa zaidi ya maneno/ nasaha zetu
Unaishi vipi na majirani zako? Je unaishi vipi na mwenzi
wako hapo ndani? Unaishi vipi na wageni?
Kama ulikuwa hujajua, basi tambua kwamba mwalimu wa kwanza wa mtoto ni mzazi,
mtoto yeyote anapokuwa hupenda kuwa kama baba/mama yake. Je anayoyaona
unayafanya ni sawa na unachomwambia afanye?
3. Kudharau Tabia za mwanzo za mtoto
Tabia yoyote anayokuonyesha mwanao katika umri mdogo, ndiyo hiyo atakayoionyesha akiwa na miaka 30!. Kama anatabia ya ubinafsi, ambayo pengine kajifunza kwa mzazi mmojawapo, shuleni nk, basi usitegemee maajabu kuwa mtoto atabadilika na kutumia neno “ni utoto”. Zijue tabia Za mwanzo za mwanao, mbadilishe mapema iwezekanavyo (kama ni mbaya) kwani akizoea itakuwa sehemu ya maisha yake na itakuwa “vita” kutaka kumbadilisha akiwa na umri mkubwa zaidi.

4. Kulea Kwa mashindano
Mara kadhaa utasikia watu wakisema mtoto wa mzee Fulani ana
afya eti tu kutokana na unene uliopitiliza. Au utasikia Shule Fulani ndio bora
kwa kuwa tu wana ada kubwa na wengine hutaka watoto wao wawe hivyo na kuenda
huko ili tu kupata heshima kumbe ni hatari kwa mwanao ama unafanya mambo
yaliyojuu ya uwezo wako unaishia kujinyima Kupita kiasi matokeo yake hutaweza
kutimiza mahitaji mengine muhimu kwa familia yako!
5. Kusahau Ibada
Kila mtoto huhitaji mazingira ya kuchagua ni mtu gani katika maisha angependa kuwa kama yeye (needs variety of role models) na hakuna sehemu salama kwa makuzi ya mwanao kama nyumba za ibada kwani licha ya kufundishwa dini, huko atafundishwa mabaya ni yapi na mazuri ni yapi pia. Mfano Utafiti unaonyesha kuwa mtoto akiambiwa ukitenda baya Fulani utachomwa moto ataacha mara moja tofauti na mtu mzima. Hivyo hata kama mzazi huna tabia ya kwenda kanisani/msikitini basi jitahidi mwanao aende.

6. Kuamini watoto wetu hawana makosa (wamekamilika)
Tatizo kubwa ninalolisikia kutoka kwa walimu, washauri,
wasichana wa kazi, au walezi wengine wa
watoto kwenye mashule na majumban ni
kwamba wazazi wengi hawapendi kusikia mambo hasi (ubaya) yanayohusu watoto wao. Wengi hudai watoto wao
hawako hivyo, wakisahau kuwa wao wametingwa na majukumu mbalimbali na hawajui
maendeleo yoyote ya mtoto!
Wa kwanza kulaumiwa huwa ni mlezi huyo na mzazi hukaa upande
wa mtoto. Matokeo yake mtoto hatamsikiliza mlezi wake tena kwani anajua mzazi
yuko upande wake!
7.Kutomsikiliza kabisa/ Kumsikiliza Kupita Kiasi
8.Kutowapa nafasi ya kucheza Utotoni
Ulishawahi kurudi nyumbani ukakuta kuta zako zote za nyumba zimechorwa vipepeo, midoli na kubandikwa
stika mbalimbali ? Je, ulichukua hatua gani? Ukweli ni kwamba hiyo ni moja ya Baraka
uliyopewa kushirikiana maisha na viumbe hawa wadogo. Siku moja hakutakuwa na michoro ukutani, wala
midoli kitandani kwako, hutasikia kelele za aina yoyote na utajiona mpweke watakapokwenda kuanzisha
familia zao.
Tunahitaji kuwapa watoto muda mwingi wa kucheza na wenzao
kwani hii huwapa nafasi ya kuzijua kalama na vipaji vyao. Pia huwapa watoto
hali ya kujiamini na kufanya maamuzi.
9.Kutokula pamoja na watoto wetu
10.Wazazi Kutokua Kitu Kimoja
Kama nilivyosema hapo juu, hakuna mwalimu wa muhimu kama
mzazi, na mtoto anahitaji malezi ya pande zote pili ikizingatiwa nae atakuwa
mzazi siku moja. Wengi wa wazazi huangalia zaidi namna ya kuwatimizia mahitaji
watoto nakusahau maisha yao binafsi.
“Prepare your child
for the road, not the road for your child"
Soma pia
sababu-kumi-kwanini-watoto-wanahitaji.malezi ya baba pia
Soma pia
sababu-kumi-kwanini-watoto-wanahitaji.malezi ya baba pia