CHONDE! CHONDE! HAKIKISHA UMESHAFANYA HAYA KABLA YA KUFIKISHA MIAKA 30.
1.Hakikisha unaijua vizuri familia yako, asili yako na ndugu
zako wote wa karibu, kama kuna ndugu yako yoyote wa karibu usiyemjua, hakikisha
mnafahamiana kabla hamjawa watu wazima zaidi.
2.Uwe umeshawahi kutengeneza kitu chako mwenyewe na kukiuza, au kuanzisha mradi au biashara yako mwenyewe
(from the scratch) na kuufanikisha. Hii itakupa kujiamini na kujiona ni wa Muhimu
na hutakuwa muoga wa kufanya maamuzi yeyote mengine magumu
3. Hakikisha umeshawahi kuwa na watu wanaokutegemea
kimaisha/ kimawazo, itakupa utayari wa kuyakabili maisha yaliyopo mbele yako
kama ndoa, watoto nk. Na hutayaogopa
maisha tena!
4. Uwe umeshawahi kumpa mtu hela yako ya mwisho kwa kuwa
alikuwa na shida kubwa kuliko ya kwako kwa muda ule. Hii inakupa nguvu ya
kuweza kujitoa muhanga kwa ajili yaw engine ambapo tayari utakuwa na hazina
kubwa kwani kwa umri ulionao, unaweza kukwama muda wowote na mtu usiyemtegemea
ndiye atakaekuwa msaada wako.
5.Kusafiri safari ndefu peke yako bila kuwa na mwenyeji,
wala mtu unayemfahamu. Kama hujawahi basi jitahidi usafiri kwenda mji mwingine,
utafute mahali pa kulala mwenyewe, uzijue barabara, mitaa, na njia za mkato za
huko, na uone tofauti ya kuishi ugenini katika jamii mpya.
6.Uwe umeshawahi kufanya maamuzi magumu au kulivaa jukumu
ambalo kila mtu analikwepa, na kutodhani kama unaweza kulikabili.
7.Uwe umeshawahi kuwa na mpenzi (au Unae), umeshawahi
kupenda, na unajua mapenzi ni kitu gani, mazuri na mabaya ya mapenzi ni yapi, njia za uzazi, mahitaji ya mtoto ni yapi,yaani
kwa ufupi, uwe na uwezo wa kuwa mume au mke wa mtu.
8.Jifunze kuvaa kwa heshima lisiwe tu suala la kupendeza. Anza
kujijali, jali afya yako, na uwe na marafiki wanaoweza kukushauri, na wapenda
maendeleo.
9.Hakikisha unajua kuweka akiba, na una hela kiasi Fulani kwa
ajili ya tahadhari
10.Unaishi kwa kujitegemea (Isiwe chumba kimoja), na
unamiliki angalau vitu vichache vya msingi nyumbani kwako.
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako