SABABU KUMI KWANINI WATOTO WANAHITAJI MALEZI YA BABA PIA
Watoto huhitaji malezi ya pande zote mbili bila kujali
wazazi wao wako pamoja au la. Wanaume wengi wamekuwa wakisahau hili nakuhisi
mama ndie mwenye jukumu pekee la kulea watoto. Mara kadhaa hurudi usiku na
kukuta watoto wamelala na hutoka asubuhi sana kabla hawajaamka pengine bila
hata kujua wameamka vipi. Zifuatazo ni sababu kadhaa kwa nini wazazi wanahitaji
malezi ya baba:
1. Kuwaelewa wanaume.
Utashangaa lakini sehemu ya kwanza ya mtoto kujua mwanaume
ni mtu gani, anaonekana vipi na tabia zake ni kupitia baba. Unavyoishi na
familia yako ndio hivyo mtoto atajua wanaume wote wako hivyo!
2. Kucheza nae
Akina baba hucheza kwa namna tofauti kidogo na watu wengine,
mara kadhaa utasikia mama akigombana na baba pengine tu baba anatumia nguvu
nyingi akiwa anacheza na mtoto akihisi atamuumiza! Akina baba hucheza kwa nguvu
zaidi na hucheza na mtoto kwa muda mrefu zaidi hii humfanya mtoto ajihisi salama
na mwenye furaha.
3. Kwa ajili ya Tabia
Utafiti unaonyesha kuwa watoto wanaolelewa na baba huwa
na tabia bora zaidi kuliko watoto
wanaolelewa na mama pekee.
4. Mtetezi wao
Hakuna kitu mtoto huhitaji akiwa mdogo kama rafiki wa
karibu. Watoto wadogo hasa wa kike hupenda sana kuwa karibu na baba yao, kwan
huhisi salama zaidi akiwa na baba nan i mtu atakayemtetea kwa mama.
5.Kujiamini
Uwepo wa baba katika maisha ya mtoto humfanya ajenge hali ya
kujiamini kwani huhisi siku zote kuna mtu nyuma yake kwa ajili ya kumtetea.
6. Kujua namna ya kuwa baba bora/namna ya kuishi na mume
Zile tabia njema
anazoziona kwa baba na mama ndio hivyo hivyo atafanya kwa mpenzi wake. Wazazi
husahau kuwa Watoto hujiskia vizuri sana wanapoona hali ya mawasiliano mazuri
kati ya wazazi wao hata wanapokua wametengana.
7.Kwa ajili ya uchaguzi wa njia sahihi
Mtoto anaelelewa na mama tu huwa na njia moja tu! Nayo ni ya
mama, ni vema mtoto kupata upendo wa wazazi wote wawili ili ajue ni njia ipi
sahihi kwake.\
8.Kuheshimu mamlaka
Kukaa na baba nyumbani humsaidia mtoto namna ya kuheshimu
mamlaka mbalimbali za mahali husika. Mfano atajifunza kuwahi kurui nyumbani,
kuvaa vizuri nk.
9.Kwa ajili ya Busara
Wanaume wanauzoefu mwingi zaidi na maisha ya kawaida hasa
kuishi na watu uvumilivu nk. Ni kawaida kumkanyaga bahati mbaya mwanaume,
ukamuomba msamaha na akakuelewa, lakini kwa wanawake wengi hadithi huwa
tofauti. Hapa utaona ni jinsi gani busara hii anavyoihitaji mtoto kuoka kwa
baba.
10. kufanya kazi kwa nguvu na bidii
Wanaume pia ni watu wanaofanya kazi kwa bidii sana hii
humfundisha mtoto kutokata tamaa .