MUHIMU:::FUATA NJIA HIZI 10 KUPUNGUZA MADHARA YA SIMU ZA MKONONI KWA AFYA YAKO!
Hakuna atakaepinga kwamba ujio wa sayansi na teknolojia
umerahisisha sehemu kubwa ya maisha yetu! Lakini unajua vifaa vya kielektroniki
vina madhara gani kwenye afya yako? Kutokana na vifaa hivi (kama simu na
kompyuta) kuwa sehemu ya maisha yetu,
imekuwa vigumu kuviepuka kwa asilimia miamoja lakini hizi ni njia fupi
za kupunguza madhara hayo.
1.Jenga utaratibu wa kutuma ujumbe mfupi
(sms) pale ambapo hakuna haja ya kupiga simu. Uwekaji wa simu karibu na Kichwa
chako kwa muda mrefu haishauriwi kiafya kwani simu huzalisha miale inayoweza
kusababisha kansa au brain tumor 2.Tumia “earphones” (visikilizio vya masikioni) wakati wa kuongea na
Simu. Hii huongeza umbali kati ya simu yako na kichwa chako. 3.Weka
Sauti Kubwa (lodspeaker) na kuweka simu mbali kidogo na sikio lako.
Hupunguza hatari ya miale ya simu kwa mwili wako 4.Epuka kutumia Simu wakati mtandao
ukiwa chini sana. Hii hufanya simu yako kutumia nguvu kubwa kupata
“network” na kukuweka kwenye hatari zaidi kwani wakati huo simu hutoa
miale zaidi. 5.Usiweke Simu sikioni kabla ya unaempigia hajapokea. Utafiti
unaonesha kwamba Simu hutumia nguvu zaidi inapotafuta mtandao kuliko wakati
mwingine wowote. Hivyo unashauriwa kutoweka simu Sikion Unapoanza kumpigia mtu. 6. Zima Simu yako inapokua haina matumizi
yoyote ya ulazima 7.Epuka kuweka Simu karibu na Kichwa Chako
Unapolala na pia Usiweke simu yako chini ya mto wa kulalia wakati umelala. 8.Jitahidi kuwa na mazungumzo mafupi
iwezekanavyo ili kuepusha hatari. . 9.Unaposafiri
hasa safari ndefu, epuka mazungumzo marefu kwani simu yako huangaika
zaidi kutafuta mtandao na hio hukuweka wewe kwenye hatari zaidi kiafya. 10.Nunua
Simu yenye SAR (specific absorption rate) ya chini zaidi. Kujua Kuhusu
SAR na zaidi juu ya utambuaji wa simu yenye ya chini zaidi bonyeza hapa Ref:life.gaiam.com