WENYE MAFANIKIO HUFANYA VITU HIVI KUMI KABLA YA SAA MBILI ASUBUHI JIFUNZE
1.Kwanza Huamka Kitandani
Wataalamu wanasema, ili uweze kutimiza ndoto ulizoziota, cha kwanza amka kitandani!

2.Huchora ramani ya siku nzima.
hakikisha unajua siku ya leo utafanya vitu gani, vingapi na kwa muda gani. Kipi kitakuwa cha kwanza na kipi ni kipaumbele.

3. Hujipa Dakika kadhaa za kutafakali.
Afya ya mwili ni Muhimu siku zote, lakini ili uwe na mafanikio unahitaji pia afya ya akili. Jipe muda wa angalau dakika 10 kwa siku kutafakari siku yako, ulikwama wapi, changamoto ulizonazo, na jinsi ya kuzikabiri

4.Hufanya Mazoezi.
Mazoezi huusaidia Mwili kuwa na utayari wa kuanza siku mpya. Sio lazima uende uwanjani au gym unaweza kufanya mazoezi hata sakafuni, juu ya kitanda nk!

5. Huwahi mapema (kazini, shuleni, biashara nk)
Wengi huwa hawalipi uzito suala hili hasa kwetu afrika, lakini ukweli ni kwamba, unapowahi kazini huifanya siku yako yote iwe bora. Na unapochelewa kazini, si tu utaharibu siku yako, bali pia utajikuta umeharibu na siku ya wengine pia.

6.huwasiliana na Watu wao kadhaa wa karibu
Hii sio tu itakusaidia kujua
wana hali gani bali pia hufanya watu wengine waanze siku yao vema kwa kuhisi ni watu Muhimu, na kuna mtu anatambua
mchango wao.
7. Hupata Kifungua kinywa
chenye afya
Sio lazima kiwe cha bei ghari, bali unatakiwa utengeneze kifungua kinywa unachomudu ila hakikisha kina virutubisho kamili. Mfano si sahihi kufungua kinywa kwa soda na biskuti.

8.Huiamini Nguvu yao ya ndani kwamba kila watakachofanya
siku hiyo kitafanikiwa
Jambo kuu katika kutimiza lengo lolote, ni kuamini kwanza uwezo wako na kuamini uwezo huo unatosha kutimiza lengo hilo!

9. Hukumbuka Msemo Huu “Maisha yasipotabasamu mbele yako,
Yatekenye mpaka mpaka yacheke!” ukiwa na maana ya kwamba, maisha yanaweza
yasionekane mazuri kwako lakini mwenye jukumu la kuyaweka sawa ni wewe!
10. Hushika Kalamu na karatasi, na kuandika chochote!
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako