SABABU KUMI KWANINI UNATAKIWA KUTEMBEA NA KALAMU YAKO! (WHY CARRY A PEN?)
1.Kujiepusha
na magonjwa mbalimbali hasa yanayotokana na bacteria yanayoweza kutokana na
kuazima kalamu au kutumia kalamu za jumuia mfano benki, mashuleni nk!
2.Kuharakisha
mambo!. Ni mara ngapi umekwenda kulipia sehemu mara karani anapoteza dakika
tano akitafuta kalamu yake? Au unajaza fomu na inabidi watu watano msubiri
kalamu moja!
3.Itakupa
uwezo wa kukumbuka vitu vidogo! Kwa mujibu wa wataalamu wa mabo ya saikolojia, ni
rahisi kukumbuka kitu unapoandika kingine. Pia hukupa uwezo wa kupambanua mawazo
yako!
4. Kubeba kalamu yako hukusaidia
kutozubaa/kulala usingizi unapokuwa kwenye mikutano au vikao mbalimbali kwan
utautumia muda wako kuwa makini kusikiliza ili upate vitu Muhimu vya kunakili.
5. Kunakiri wazo
Muhimu unalolifikiria. Ukifanya hivi kila siku utajikuta una hazina kubwa sana
ya mawazo mazuri na kubadili maisha yako!
6.
Hukuongezea ubunifu hasa unapokuwa mpweke au umechoka, jaribu kuchora vidoti
mbalimbali, viunganishe kwa namna mbalimbali, utajikuta umepata wazo Fulani ambalo
pengine halikuwemo kichwani mwako.
7.Hukuongezea
wasifu wako mbele za watu. Licha ya kalamu yako kukupa uchangamfu, pia kalamu
hiyo hiyo itakufanya uonekana mtu makini na muelewa
8.Kuandika
mawasiliano ya mtu kwa haraka zaidi mfano barua pepe, link ya website nk!
9. Kuandika
nukuu muhimu kwa haraka vitu unavyoambiwa unapoongea na simu!
10. Inaweza
kuwa silaha hasa pale unapotaka kujihami hasa mbele ya wezi, wakabaji.
“A
pen is a tongue of the mind!”
SURE MAN.WELL SPOKEN.
ReplyDeleteThanks Man!
DeleteSawasawa
ReplyDelete