EPUKA KUTUMIA MANENO HAYA UNAPOMFARIJI MTU ALIYEFIWA
1.Usijali, Utapata mtoto mwingine (unasahau kuwa kila mtu
ana nafasi yake duniani)
2.Jifunze kusahau bwana, Mbona umepita muda mrefu toka atutoke
3.Tulimpenda ila Mungu Kampenda zaidi (Hili neno halizoeleki
jamani, yaani unahalalisha kuondoka
kwake)
4.Shukuru aliishi Maisha Marefu, wengi wanakufa mapema
5. Najua inavyouma, ila usijali utamsahau tu
TUMIA MANENO HAYA
1.Pole sana, Nashindwa hata nitumie neno gani ili ujue
nilivyoguswa na suala hili zito
2. Hatutomsahau Kamwe/ Pengo lake halitazibika
3.Mpe pole na Kumuahidi utakuwa nae kipindi chote hiki
kigumu, akihitaji kitu utakuwepo kwa ajili yake
4.Mkumbatie bila kusema chochote
4.Mkumbatie bila kusema chochote
5.Kaa nae karibu tu na umpe mahitaji Muhimu, kumuomba ale
nk.
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako