FAIDA KUMI ZA HUGGING (kukumbatia). ANZA LEO!
1.Husaidia uzalishaji wa homoni ya “oxytocin” ambayo husaidia sana mwili kuondoa tatizo la
kuhisi upweke, hasira, na kutengwa.
2.Unapomkumbatia mtu, unaupa mwili hali ya kujihisi salama na
huru pia.
3. Hug hufanya misuli isinyae hivyo kusaidia
kuondoa/kupunguza baadhi ya maumivu ya mwili na kuufanya uwe huru.
4.Huboresha mahusiano ya watu wanaopendana kwani
unapomkumbatia mtu unaonyesha hali ya kupenda, usalama, na mapenzi ya dhati.
5.Huondoa uoga na wasiwasi.
6.Utajikuta unajiona wa thamani kumbuka tulipokuwa wadogo, wazazi wetu walitukumbatia
na tukajiona tunapendwa na tuko mahali salama, upendo ule tulioonyeshwa na
wazazi wetu, unakuwepo ndani yetu kadri tunavyokuwa watu wazima, na
unapomkumbatia mtu inakufanya uhisi kupendwa na wathamani.
7.Huleta usawa kwenye Mfumo wa fahamu kwani wengi wetu
tunaishi katika mazingira yanayoufanya mwili kuwa katika hali ya kujihami muda
wote hivyo unapomkumbatia mtu, mwili husinyaa na kurudi katika hali yake ya
kawaida.
8.Hug hutufundisha kutoa na kupokea.
9.Hushusha shinikizo la damu mwilini, Mgusano wa mwili
husababisha neva za kwenye ngozi zinazoitwa “Pacinian corpuscles” kupeleka
habari kwenye sehemu ya ubongo (vagus nerve) inayohusika kushusha shinikizo la
damu.
10.Watoto wanaokumbatiwa kwa kiasi kikubwa wakiwa watoto,
huwa katika hatari ndogo zaidi ya kupata msongo wa mawazo kuliko watoto
wasiokumbatiwa vya kutosha.
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako