YAJUE HAYA KUMI KABLA YA KUSAFIRI AU UNAPOKUWA NJE YA NCHI KWA AJILI YA MASOMO/KAZI/KUISHI NK.

YAJUE HAYA KUMI KABLA YA KUSAFIRI AU UNAPOKUWA NJE YA NCHI KWA AJILI YA MASOMO/KAZI/KUISHI NK.

1.Jitahidi uwe na mizigo michache iwezekanavyo, usibebe nguo nyingi! Kumbuka hutavaa nguo hizo zote. Kuwa na begi linalobebeka na ukiliwekea label itakua nzuri zaidi.

2. Jifunze maneno machache ya lugha ya nchi unayotembelea (kumbuka sio kila nchi wanajua kiingereza) maneno ya Muhimu ni kama salamu, msaada, ndio, hapana nk.

3. Kwenye suala la mawasiliano, tumia app kama whatsapp na viber. Hizi ni rahisi kutumia, na utawasiliana na watu wote (nyumbani na ugenini)

4.hifadhi majina yako Muhimu, anuani, na namba za simu kwenye “google docs” hii itakusaidia hata ukipoteza simu, mkoba nk.

5.Jifunze mfumo wa pesa wa nchi unayokwenda kwa haraka kuepuka kuhangaika unapotaka kufanya manunuzi

6.Tengeneza marafiki wapya kwa haraka zaidi, itakufanya uzoee maisha kwa haraka na ni nzuri kwa usalama wako pia!

8.Jaribu vyakula aina mbalimbali, hata usipovipenda kwa wakati huo usijali, utapata kinachokufaa baada ya muda mfupi

9.Ukifika hakikisha unajua ubalozi wa nchi yako uko wapi, na kama kuna raia wenzako wa afrika mashariki wajue pia. Itakufanya ujihisi nyumbani


10.Kumbuka licha ya vikwazo vingi utakavyokumbana navyo, kuna muda utafika utatulia na maisha yako yataendelea kama kawaida.

soma pia

1 comment:

  1. Kubeba mizigo michache muhimu maana mwingine anafungasha hadi ubebaji unaguwa tabu

    ReplyDelete

Toa maoni yako

Copyright © 2014 Kumi Muhimu