LAZIMA UTAKUTANA NA HAYA 10 UKISHAFIKIA MIAKA YA 20 (Watanzania wengi Hatuyajui)
1.Tegemea kukutana na kipindi kigumu cha kukosa fedha,
wazazi hawatakuwa karibu na wewe sana kama ulipokua mdogo. Jiandae kujifunza
kupambana na kutimiza baadhi ya mahitaji yako.
2. Utaangukia pua mara kadhaa pengine kutokana na kazi,
mapenzi, elimu nk. Cha Muhimu ni kuamka haraka iwezekanavyo na kujifunza
kutokana na makosa
3.Usitegemee kuishi eneo moja (pengine ulilozaliwa) Tegemea Kutengana na marafiki zako wengi wa zamani
pengine kutokana na kubadili eneo la makazi, shule, kazi nk vitakavyokuchukulia
muda wako mwingi na utapata marafiki wapya (isikupe shida)4.Katika muda huu, utakuwa na vitu vichache sana vya kudumu
kuanzia makazi, marafiki au hata kazi. Jiandae kwa hayo kwani ushakuwa mtu
mzima.
5. Utakutana na Watu wengi zaidi wanaopingana na wewe. Pengine
itakufanya usijiamini tena lakini ndio hali halisi, ikabili! kwani ukishindwa,
huu ndio mwanzo wa kuyaogopa maisha na kuwa masikini.
6. Kwa mara ya kwanza tegemea kukutana na ugumu wa maisha
(uso kwa uso). Kile ulichukuwa ukikisikia kinaitwa “Changamoto” sasa kiko
mlangoni japo changamoto hizo hazitakuja kwa haraka au kwa wakati mmoja.7. Wazazi au ndugu zako wa karibu watakuacha ufanye baadhi
ya mambo mwenyewe, ule ukaribu wao kwako utapungua na kuna wakati utajihisi
mpweke sana lakini sasa unahitaji ubadili namna yako ya kawaida ya kufikiria.
8. Sio kila mtu atakupenda, pengine hutaona unavutia tena, hivyo ni vema ujue uwezo na udhaifu wako ili
usitetereke.
9. Mwili wako utabadilika kwa kiasi Fulani, pengine kwa
kupata fedha, kukosa kipato, mawazo, mapenzi, kupata mtoto nk. Hivyo jiandae
kwa hali zote. Usitegemee kubaki kama ulivyokuwa.
10. Mpenzi uliyenae ni nadra kuja kuoana nae kwani ni Watu
wengi sana wataingia maishani mwako kwa namna nyingi na kwa nia tofauti na
umeshafika umri wa kuamua na kuchagua.“Falling doesn’t matter, what matters is how much time did
you take to get up.. Remember pain is inevitable in life, but suffering is
always optional”
© Kumi Muhimu 2014
Soma pia
duu bora wajue mapema
ReplyDelete