MAAJABU KUMI (10) AMBAYO HUJUI KAMA MWILI WAKO HAUWEZI KUYAFANYA

MAAJABU KUMI (10) AMBAYO HUJUI KAMA MWILI WAKO HAUWEZI KUYAFANYA

10. Huwezi Kuandika Namba Sita ukiwa unazungusha Mguu wako wa Kulia mwelekeo wa Saa (clockwise).Kaa kwenye kiti, Nyanyua mguu wako wa kulia juu, kisha anza kuuzungusha kwa duara kwa kufuata muelekeo wa saa (yaani kutoka kushoto kwenda kulia) endelea kufanya hivyo huku unaandika nambasita (6). Umegundua nini? Mguu wako umegeuka na kuanza kuzunguka muelekeo wa kushoto!!


9. Huwezi kurusha Mate ukiwa umeachama mdomo!



8. Huwezi Kunyanyua Kidole Chako cha Pete Katika hali ifuatayo;


Kunja kidole chako cha katikati juu ya meza ukiviacha vidole vyako vinne vikiwa vimenyooka kama inavyoonekana kwenya picha kushoto. Jaribu kunyanyua dole gumba, kisha nyanyua kidole kinachofuata, na kidole kidogo cha mwisho... rahisi sio?? SASA nyanyua kidole cha pete... kimegoma!

7. Huwezi Kuchezesha Pua yako kulia na kushoto


(Sijasema ujaribu kufanya zoezi hili)



6. Huwezi Kuokota kitu chini ukiwa umeegamia ukuta na visigino vyako vimegusa ukuta huo

fanya zoezi lifuatalo; Simama ukiwa umenyooka huku sehemu ya nyuma ya miguu yako (visigino) vikiwa vimegusa ukuta. jaribu kuokota kitu mbele ya miguu yako!


5. Huwezi Kutikisa Sikio lako

ukijaribu utajikuta kichwa chako kinainama muelekeo wa sikio ulilojaribu kutikisa!


4. Huwezi Kupiga Chafya bila Kufunga Macho!



3. Huwezi Kujitekenya


2. Huwezi Kufanya Zoezi lifuatalo;
Egemea ukuta kwa kutumia ubavu wako wa kushoto ukiwa umenyooka, sogeza mguu wako wa kulia pembeni kidogo, kisha jaribu kunyanyua mguu wako wa kushoto!..

1. Nakuachia wewe Tuaambie Ni Kipi mwili Wa binadamu Hauwezi Kufanya!



Kwa maoni na ushauri, Tuandikie kupitia  kumimuhimu@gmail.com, (0) 769 640 408
Copyright © 2014 Kumi Muhimu