1.Ukiamka tu asubuhi, cha kwanza ni Kushika simu yako na kuangalia ni nani
kakutumia meseji, ame comment picha yako, au Ulichokiandika kwenye facebook
kimepata “likes” ngapi!
2. Una marafiki zaidi ya 100 ambao hamjawahi kuonana
3. Unatumia alama ya “@” na “#” hata unapoandika sms ya kawaida!
4. Una “like” picha zako Mwenyewe hata kama ulipost mwaka
jana ili tu watu wazione
5.Unatumia sana Vifupi kama 2 (too), u (you) LOL (laugh out Loud) YOLO (You only live once)
IDK (I don’t know) na unahisi kila mtu
anajua!
6 Usipoonekana facebook wiki moja lazima upigiwe simu na
marafiki zako kama unaumwa au la
7. Mtu akikuchekesha unatumia neno “lol” badala ya kucheka!
8. Chakula unachokula hakiendi tumboni tu, bali pia huenda
dacebook, twitter, instagram nk!
9 Una “minimize” ulichokuwa unakifanya kila ukimuona bosi! Hata
kama ulikuwa unafanya kazi yake J
10 Asubuhi: “good
morning facebook” mchana: “Mchana mwema
wadau karibuni chakula”
Jioni: “Daah nimechoka kweli” Usiku:”Goodnight jamani”
0 comments:
Post a Comment
Toa maoni yako