USIKIMBILIE KUWA MZAZI YAJUE HAYA KUMI MUHIMU KWANZA.

USIKIMBILIE KUWA MZAZI YAJUE HAYA KUMI MUHIMU KWANZA.

1.Maisha yako yatabadilika moja kwa moja! Utajifunza matumizi mazuri ya fedha, ulaji, kuendesha gari kwa hekima, Mahusiano na mpenzi wako yatabadilika (kwa uzuri au ubaya) mtajiona wa tofauti sana. Muda wako wa ziada utapenda ulale kwani kukosa usingizi halitakuwa jambo la ajabu.

2.Utatakiwa upende anachopenda Mtoto.
Sahau kuhusu timu yako uipendayo kwa muda, kipindi chako ukipendacho, utajua machache sana yanayoendelea duniani, na sasa utapenda anachopenda mtoto. Utakuwa mtoto kwa muda, hii ni kawaida sana.


3.Nyumbani Kwako kutakuwa kijalala Kidogo
Watoto wanapenda michezo mingi sana! Usitegemee kukuta sebule yako ni safi muda wote kama ulivyozoea, usifikirie kwamba atavijali vitu vyako kama unavyojali wewe.







4. Simu/ Computer yako itakuwa ya mwanao.
Licha ya juhudi zote jua ya kwamba watoto watagusa simu, au computer  yako tu! Watapenda kuwa na wewe, kufanya kazi kama wewe, na kutumia vitu vyako. Hakikisha vitu vilivyo kwenye simu, au computer yako vinamfaa, na hakuna ubaya akiona.

5.Utaanza Kujiona na kuona Makosa uliyoyafanya ukiwa mdogo, utaijua thamani yako na ya wazazi wako ambao pengine hawatakuwepio.




6.Hutaweza tena Kutumia fedha kwa ajili yako mwenyewe kwani utaona kila fedha unayotumia, ungeweza kutumia na familia nzima. Na utajisikia raha zaidi kumnunulia mwanao kitu zaidi ya kujinunulia wewe mwenyewe.

7.Suala la Muda litabadilika, na utalaumiwa zaidi na watu wako wa karibu kwamba hujui kutunza muda. Usitegemee kujiandaa kwa haraka unapotoka kama zamani.


8.Miezi Michache ya mwanzo baada ya kupata mtoto, kitakuwa kipindi kigumu zaidi kuwahi kukutana nacho, ratiba zako za kulala, kuoga, kupika, kusali nk zitabadilika kabisa. Utapitia vipindi vigumu, utakosa fedha ila hakuna namna tena.

9.Rafiki wako wa karibu atakuwa Daktari au Muuguzi wa mwanao. Utazijua hospitali nyingi zaidi kuliko bar, na kumbi zako za zamani za kustarehe.


10. Jiandae kwa dharula za aina zote, hakikisha una fedha ya dharula au wakati mwingine itakubidi uhamishie ofisi nyumbani ili uweze kuendelea na shughuli zako za kila siku.




USIKIMBILIE,JIANDAE


0 comments:

Post a Comment

Toa maoni yako

Copyright © 2014 Kumi Muhimu