KAMA UNAFANYA HAYA BASI WEWE NI MMOJA KATI YA WATU WANAOUDHI ZAIDI KWENYE DALADALA
1. Kulala ndani ya daladala na kumuegamia mtu wa jirani,
unamkwepa anashtuka na baada ya dakika moja anakuegemea tena! Mbaya zaidi
anatoa harufu mbaya kukohoa na kupiga chafya bila kujizuia.
2. Harufu mbaya. Umepanda gari ghafla anaingia mtu kabeba mzigo
wa samaki. Anaingia nao ndani na kukaa karibu na wewe. Au umekaa na mtu pembeni
anaimba/kuongea na anatoa harufu kali mdomoni!
3.Mtu anaongea sana na kukulazimisha umsikilize. Au anataka
kila mtu ndani amsikilize yeye. Anaongea kwa sauti kubwa na wakati mwingine,
mate yanatoka kinywani.
4. Mmefika kituoni, ghafla anatoka mtu kutoka nyuma
anapita kwa nguvu na kumkanyaga kila mtu na hasemi/ hakusema kama anashuka.
5.Mtu anakukodolea macho toka mwanzo mpaka mwisho wa
safari. Kumzuia mtu huyu, na wewe mtazame sehemu mojawapo ya mwili wake(isiwe
usoni ). na atakosa ujasiri huo tena!
6. Matusi. Uko kwenye usafiri na mzazi au mwanao, ghafla watu wanaanza
kuporomosheana matusi ya nguoni. Kwa kweli watu hawa huudhi sana.
7.kuchunguza simu ya mtu mwingine. Umekaa kwenye siti
kuna mtu amesimama nyuma yako anachunguza kila unachokifanya kwenye simu yako,
ukisogeza pembeni nayeye yumo!
8.Kuongea na Simu kwa sauti ya juu na kuanza kuongea
mambo yako ya ndani, kujisifu au kutishia. Si kila mtu anataka ajue siri zako au pengine
uwezo wako.
9.kula kwenye daladala. Umepanda na mtu amenunua muhindi,
karanga, miwa nk na anaanza kula na kusababisha baadhi ya mabaki kukuangukia
10. Muziki. Si kila mtu anapenda aina ya muziki
unayopenda wewe. Inaudhi umekaa na mtu
amefungulia simu yake muziki kwa sauti au mahubiri ya dini Fulani kwa
sauti kwa lengo la kuwaudhi watu wa dini nyingine!