UNAYAJUA MAAJABU HAYA 10 KUHUSU MICHUANO YA UEFA? (UEFA CHAMPIONS LEAGUE)
1. Arsenal wanashikilia rekodi ya kuwa timu pekee
kucheza mechi ya UEFA ikiwa na wachezaji 11 wa mataifa 11 tofauti. Yaani kila mchezaji
alikuwa na taifa lake!
2.Real Madrid inashikilia rekodi ya kuchukua kombe
mara nyingi zaidi ikiwa imechukua mara 10. Pia ikiwa timu iliyochukua kombe
mara tano mfululizo (wakati likiitwa “European cup”) kuanzia mwaka 1956 mpaka
1960
4.Ni wachezaji wawili tu waliowahi kuoneshwa kadi
nyekundu katika mchezo wa fainali ya uefa Jens Lehmann (Arsenal) katika fainali ya 2006 na Didier Drogba
(Chelsea), Timu zao zilipoteza michezo hiyo.
5. Klabu za Hispania ndio zinaongoza kuchukua
kikombe cha uefa mara 14 (real madrid na barcelona pekee). Wakifuatiwa na
vilabu vya England na Italia mara 12.
6.Benifica inashikilia rekodi ya kushinda magoli
mengi zaidi katika mechi mbili za hatua ya mtoano ilishinda jumla ya mabao 18-0
dhidi ya Dudelange. Mechi ya kwanza benifica ilishinda 8-0 na mechi ya pili
10-0
7.Atletico Madrid imefika fainali ya uefa mara mbili tu, ya
kwanza ikiwa mwaka 1974 dhidi ya Bayern munich ambapo mechi iliisha kwa sare ya
moja kwa moja na kuamuliwa irudiwe siku mbili baadae na Bayern kushinda 4-0. Ya pili ilikuwa ya mwaka 2014 ambapo walicheza
dhidi ya r.madrid na real kushinda mabao 4-1.
8.Mchezaji mkubwa zaidi kucheza UEFA ni Marco Ballotta wa lazio akiwa na miaka 43 huku
mchezaji mdogo zaidi kucheza uefa akiwa
ni muafrika Celestine Babayaro akiwa na miaka 16!
9.Mwaka 1967 Celtic ilibeba kombe ikiwa na wachezaji
wote wazaliwa wa eneo moja la kilometa 50 kuzunga uwanja wao wa nyumbani.
10.Goli la mapema zaidi kufungwa lilikuwa la
mchezaji wa Bayern muchen Roy Makaay, sekunde 10 tu baada ya mchezo kuanza!