MAMBO KUMI (10) YA KUFANYA KUJIKINGA NA DENGUE

.
Mambo Kumi (10) Ya Kufanya Kujikinga Na Dengue
- Epuka Kuvaa nguo fupi kama kaptura, shati au tisheti kata mikono. Vaa suruali na shati/sweta la mikono mirefu
- Usiweke Makopo chini ya Viyoyozi kwan hudondosha maji yanayoweza kuwavutia mbu
- Maji ya kwenye makopo ya maua yabadilishwe mara kwa mara
- Epuka Kuanika nguo Mbichi ndani ya nyumba. Hii huwavuta mbu kuzaliana
- Osha vyombo visivyotumika angalau mara moja kwa wiki
- ondoa madimbwi yoyote yanayotuwamisha maji
- Tumia chandarua unapolala nyakati za mchana
- Funika makopo ya taka ili kutowavutia mbu
- Kunywa maji mengi na jenga mazoea ya kunywa juice za matunda
- Usiache milango wala madirisha wazi bila sababu ya msingi.
Kwa maoni na ushauri, Tuandikie kupitia kumimuhimu@gmail.com, (0) 769 640 408