WENGI HATUYAJUI HAYA KUHUSU UKUTA HUU WA CHINA “Great Wall of China”
1.Ulianza kujengwa miaka 2000 iliyopita, mpaka sasa una urefu wa kilometa zaidi ya elfu sita (6000 km)
2.Ndio Ujenzi pekee wa binadamu ulio mrefu zaidi duniani
kote. Wachina walijenga kwa ajili ya usalama wao hasa kujikinga na maadui
kutoka upande wa kaskazini.
3.Ukuta huu una upana wa mita tisa tu (30ft) ambayo ni sehemu nzuri ya kutembea kwa miguu na kuna maeneo mengine, ni salama hata kuendeshea gari.
4.Ukuta Huu ulijengwa na watumwa na wanajeshi kwa awamu
mbalimbali na zaidi ya watu milioni moja walifariki katika ujenzi huo
5. Ukuta wa china ndio shughuli pekee ya binadamu inayoweza
kuonekana kutoka anga za juu. Ila si kweli kwamba wansayansi waliuona ukuta huu
kutoka mwezini.
6.Katika hatua za mwanzo, Unga wa mchele ulitumika
kuunganishia matofali (kama gundi) wakati wa ujenzi
7.Zaidi ya watu milioni 10 hutembelea eneo hilo maarufu kwa
utalii
8. Eneo linalotembelewa zaidi na watalii ni eneo la Badaling
karibu kabisa na jiji la Beijing. Eneo hilo limejengwa miaka 2000 baada ya kuanza
kwa ujenzi huo mwaka 1957.
9.Jina la China lilitokana na sehemu ndogo ya ukuta huo
iliyokuwa ikiitwa Qin Shi Huang, ambapo “Qin” inatamkwa “chin”
10. Toroli (Wheelbarrow) liligunduliwa na wachina katika
ujenzi wa ukuta huu maarufu duniani
Soma Pia
Mambo-kumi-10-usiyoyajua-kuhusu-adolf.Hitler
Soma Pia
Mambo-kumi-10-usiyoyajua-kuhusu-adolf.Hitler
asante mkuu wabongo wengi hawana time ya kufuatilia vitu kama hivi
ReplyDelete